ACHE YESU, AWE WA KWANZA KUKUHURUMIA.

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo.

Ni jambo la kawaida kila mmoja wetu kuijali kwanza hali yake binafsi, na si dhambi kufanya hivyo, japo hilo halitufanyi tuonekane kuwa wa maana sana mbele za Mungu. Kuna wakati Bwana Yesu aliitisha mkutano mkubwa sana, pengine eneo la mjini lilikuwa ni dogo la kuuketisha umati mkubwa wa watu, au pengine palikuwa na usumbufu fulani ambao ungewafanya watu wasimsikilize vizuri, Hivyo akaamua kuwaitisha eneo la mbali kidogo na mji, mahali ambapo hapana makazi ya watu, eneo la nyika tupu, mahali ambapo hakuwaandalia mahema ya kukutania wala hakuwachagulia penye miti mingi, ambapo walau wangekaa chini yake wapate uvuli, bali alichagua eneo la jangwa lenye nyika tupu.
Na mkutano huo ulikuwa ni Mkutano wa siku tatu..

Lakini Biblia inatuambia wengi waliposikia habari ile wakatoka mbali sana, wakaenda eneo hilo la jangwa ili kwenda kuyasikiliza maneno ya uzima ya Bwana Yesu. Watu wale walifikia pengine asubuhi sana na mapema, wakijua kuwa siku zote tatu zitakuwa ni siku za kufunga, za kumsikiliza tu Bwana Yesu si vinginevyo, hivyo walifika mahali pale wakilijua hilo asubuhi sana, wakakaa chini kwenye jua lile, kuanzia asubuhi mpaka jioni,..

Jaribu kutengeneza picha, masaa 12 ya mchana wanamsikiliza tu Bwana Yesu akiwafundisha, na usiku vivyo hivyo.. siku ya kwanza, siku ya pili, mpaka siku tatu zinakwisha, wamekaa tu pale, nyikani wakimsikiliza Bwana Yesu kwa makini bila kuondoa miguu yao, huku njaa zikiwauma, lakini waliona kile wanachokisikiliza ni Zaidi ya chakula cha mwilini.. Walijua mtu hawezi kuishi kwa mkate tu, bali kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Bwana..

Embu tengeneza tena picha Bwana alikuwa anajua kabisa watu wale, walikuwa katika hali ngumu kweli kweli katika eneo lile la ukame na jua kali, alijua kabisa walikuwa hawajala kwa muda wa masaa mengi sana, alijua kabisa hali zao zinakaribia kuwa mbaya..lakini aliendelea kuwafundisha bila kuwahudumia kwa lolote, kwasababu aliona utayari wao wa kumsikiliza yeye bila kuchoka, mpaka siku tatu kamili zilipokwisha..

Lakini siku ile alipomaliza kuwafundisha, biblia inatuambia Bwana Yesu hakuwaacha hivi hivi waondoke waende zao katika hali zile za njaa bali aliona umaskini wao, aliona njaa zao, aliona mateso yako, aliona kiu yao, aliona mahitaji yao na pale pale maandiko yanatuambia AKAWAHURUMIA: embu tusome:

Katika siku zile, kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, nao wamekosa kitu cha kula, akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Nawahurumia mkutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula; nami nikiwaaga waende zao nyumbani kwao hali wanafunga, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka mbali. Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani? Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano. Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia. Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga.

Katika siku zile, kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, nao wamekosa kitu cha kula, akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Nawahurumia mkutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula; nami nikiwaaga waende zao nyumbani kwao hali wanafunga, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka mbali. Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani? Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano. Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia. Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga.

Mark 8:1-9 SUV

Unaona hapo? Walipaswa waondoke vile vile, lakini kwa jinsi alivyoona “WAMEKAA NAYE” siku zote tatu bila kuondoka uweponi mwake, bila kwenda kuhangaika hangaika kuyajali maisha yao, familia zao, biashara zao, miradi yao, ili wapate chakula wao na Watoto wao, badala yake wamedumu pamoja naye kwa siku kadhaa bila kuchoka basi tukio hilo lilimfanya Bwana Yesu AWAHURUMIE hata kwa yale mengine waliyoyakosa..

Na kama tunavyosoma kitu gani kilifuata. Wote walishibishwa mikate wakiwa pale nyikani, wakapata na ya kuondokea, mpaka ikabaki na wale samaki vivyo hivyo…Sasa unaweza ukafikiri Bwana Yesu aliwashibisha pale tu. La! Alikuwa anawadhihirishia kuwa baada ya pale na Maisha yao pia yatabarikiwa kwa mfano ule ule wa vikapu, na wala hawatapungukiwa kabisa…Lakini hiyo yote ilikuwa ni kwasababu ya yale maneno ya uzima waliokuwa wanayasikia bila kuchoka ndio yakazaa vikapu vile vya mikate na baraka walizoziendea baada ya pale.

Na sisi tujiulize, Je tunaweza kufikia hatua kama hii ya hawa watu?…Je tunaweza kuwa tayari kufunga kutokula kwa ajili tu ya kuutafuta uso wa Bwana kwa kipindi kirefu?, Je tunaweza Kufunga mihangaiko yetu, na shughuli zetu tukatenga wakati wa kuhudhuria ibada na semina ndefu za Neno la Mungu? kwa kutokujali eneo lenyewe, kutokujali mazingira yanaruhusu kiasi gani, kutokujali umbali, kutokujali hata uzima wako na afya yako? Ikiwa tu tutaalikwa mahali ambapo tumewekewa mahema, chini kuna vivuli, lakini bado hatutakwenda ikiwa tunayo makanisa mazuri tena mengine yana feni lakini hatuwezi kukaa hata masaa 2, Je tutawezaje ikiwa tutalikwa mahali penye njika tupu kama pa hawa watu? Na wakati huo huo bado tunataka Bwana Yesu azihurumie hali zetu?

Mungu anatuambia tumkaribie yeye na yeye atatukaribia sisi (Yakobo 4:8)..Hivyo tukiwa hatupo tayari kujinyima nafsi zetu na kujitesa katika kuutafuta uso wa Mungu kwa bidii, katika kuutafuta ufalme wake na haki yake, basi tujue itakuwa shida sana kuyaona matendo makuu ya Mungu maishani mwetu.

Usikazane kutafuta kujihurumia kwanza wewe unapoutafuta uso wa Mungu, subiri kwanza Bwana akuhurumie yeye, jukumu letu ni kuutafuta uso wa Mungu kwa bidii mengine tumuachie yeye, kwasababu anajua shida zetu, na mahitaji kabla hata sisi hatujamwambia. (Mathayo 6:32).

Bwana atusaidie katika hilo. Na atujalie tuchukue hatua zinazostahili katika hilo.

Pastor Boniface Evarist
GoodVine Church

Message Boniface Evarist on WhatsApp. https://wa.me/message/XLSAYATCTSESC1

USIOGOPE

USIOGOPE

Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
ISAYA. 43:1

Wakati mwingi katika maisha tunayoishi vimejitokeza vitisho ambavyo vinamfanya mtu aanze kuogopa au kutishika kuthubutu kuanza Jambo alilokusudiwa kufanya na Mungu.

Ukiona wazo lolote limekuja kichwani mwako na hilo wazo linaoneonekana kutokana na Neno la Mungu tambua unapaswa Kulifanya Tena kwa viwango vya ubora wa hali ya juu.

Si jambo rahisi kabisa kutekeleza jambo ambalo litakupa kumfurahisha Mungu, kufurahisha watu na familia yako. Hapo ndipo vitisho vilipojificha na vinakusubiri uanze au ujaribu kugusa hilo.

Utaanza kusikia kelele za mawazo yako na wanadamu, kelele zote zinakusudia kusema huwezi, usijaribu, acha, utapoteza muda, ukishindwa, shauri yako na maneno yanayofanana na hayo.

Mimi Mchungaji Boniface nakuambia hivi tazama hili Neno la Mungu linasema;

Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.

Ee Yakobo (kwa Mimi nasoma hivi Ee Boniface) na anaposema Ee Israeli (Mimi nasoma hivi Ee mpendwa wa Mungu). Nisiogope kufanya jambo ambalo linatokana na maono niliyopewa na Mungu hata Kama Kuna uzito kiasi gani.

Inawezekana wewe sio mtu wa kuajiriwa bali unatakiwa uanze Jambo ambalo litawatengenezea wengine ajira. Uanze jambo ambalo hakuna hata mmoja amewahi kufanya katika familia yenu.

Bwana anasema amekuita kwa jina lako, nikuambie hivi acha woga, simama ukijua Bwana amekukomboa ili ufanye mambo makuu na sio ya kawaida kawaida kama ambao hawajakomboa na bado hajawaita.

TANGAZA:
Mimi nimekombolewa na Mungu kwa damu ya Yesu Kristo pale msalabani, sizuiliwi Wala kuogopa chochote maana nimeitwa na Mungu na nimefanyika kuwa Mali ya Mungu. Sitashindwa wala kukata tamaa kamwe kutimiza ndoto yangu.

J!Boniface Evarist
GoodVine Church.
+1 619 800 1920
+255 752 122 744

Namna Ya Kutumia Neno Kama Ukiri Wa Kinabii

Biblia inatuambia kwamba “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi”. (Mithali 18:21) Kile tunacho kiongea, kiwe chanya au hasi, lazima kilete matokeo ya aina fulani. Tunachotangaza lazima kizae matunda.

Yakobo anatukumbusha kuwa ndimi zetu zina nguvu – na kile tunachotamka kwa vinywa vyetu kina nguvu ya kuongoza maisha yetu. (Yakobo 3:3-5)

‘Ee Bwana, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele.’ (Ps 119:89)

Kutangaza Neno la Mungu ni njia yenye nguvu ya:

  • Kuimarisha imani zetu (Warumi 10:17)
  • Kusaidia kufanikiwa katika matarajio yetu
  • Be a weapon in times of spiritual warfare
  • Kuwa silaha wakati wa vita ya kiroho (Waefeso 6:17)
  • Kusaidia kutuweka katika hali ya kutimiza kusudi la kuishi kwetu.

Namna ya Kugeuza Neno kuwa Ukiri wa Kinabii

Neno linakuwa la kinabii pale linapozungumzia nia ya Baba wa mbinguni na kusudi lake kwa maisha yetu.

Yafuatayo ni baadhi ya Mawazo yatakayokusaidia kubadilisha msitari wa Biblia kuwa ukiri wa imani:

1. Chagua mstari wa Biblia ambao

  • Mungu amesema jambo juu yako, au
  • Linalingana na kile Bwana amesema Kuhusu wewe
  • Unahusiana na hali unayopitia kwa wakati huu au maisha yako kwa ujumla au wito wako.

Kitendo cha kutangaza au kukiri Neno la Mungu kina nguvu sana, lazima utaona mpenyo wa ajabu sana kwa maana Mungu si muongo kwa ahadi zake.

2. Jiweke katika uhusika.

Unapobadilisha uhusika na kujiweka wewe unafanya iwe sauti ya Mungu kwako. Ukitazama ukiri ninaowapa kila siku utagundua tunawezaje kujiweka katika uhusika wa Neno.

3. Mara nyingi tumia wakati uliopo na ujao – kwa kufanya hivyo unabadilisha hali ya sasa na ya siku zijazo kuwa vie utamkavyo.

4. Ukumbuke huo mstari au uandike mahali na tumia hilo Neno kutangaza.

‘Heri mtu … Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku..’ (Zaburi 1:1-2)

Nimegundua kuwa kutangaza au kukiri kwa sauti na ujasiri kuna nguvu sana hasa wakati wa swala la vita au mpenyo (mafanikio). Ingawa, Hatuhitaji kutangaza au kukiri kwa sauti kubwa mara zote ili ukiri utimie. Kwa kiebrania “kutafakiri” kuna maanisha pia kujisemesha mwenyewe – na hili linaweza kufanyika kimyakimya au kimoyomoyo

Zingatia Ukiri huu kama mifano ya somo hili: