Ukiri wa kinabii ni tamko ambalo lina uzito wa mamlaka ya kifalme nyuma yake.

‘Kinabii’ inamaanisha yameundwa kulingana na mapenzi ya Mungu. Roho Mtakatifu ameelezea kusudi la Baba yako na unazungumza kile amekufunulia kwa njia ya kutangaza.

Biblia inasema tunachokitamka kina nguvu – Mithali inasema “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi”. (Mithali 18:21)

Ukiwa na ufahamu ambao umepokea katika uhusiano wako na Mungu, unaweza kutoa matamko ya kutoa uhai ambayo yanaachilia rasilimali na kufungua mpenyo wa mafanikio.


HATUA SABA ZA KUFANYA UKIRI WA KINABII

  1. Kaa katika nafasi yako ya kifalme.

“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.” ‘Warumi 8:29-30’

Ukiri ni amri ya kifalme, hivyo hatua ya kwanza kabla ya kufanya ukiri wa kinabii lazima ujitambue kuwa wewe ni mwana wa Mfalme wa wafalme. Ili kutangaza ukiri wa kinabii lazima ujitambue kuwa wewe ni nani na u mali ya nani.

Endapo hili bado unaliona kuwa ni jambo gumu basi nikuombe, ingia kwa imani katika nafasi ya kifalme, Haijalishi unajisikiaje. Tafakari Kuhusu kile Mungu amesema kwa habari yako. Ukiwa unafanya hivyo mtazamo wa zamani utaondoka, kwa kuwa wewe ni mwana wa Mungu na una vinasaba (DNA) vya kifalme katika ulimwengu wa roho.


  1. Baini nia ya Baba.

Bwana Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kufanya ukiri huu katika maombi: ‘Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.’ (Mathayo 6:9-10) au tukiiweka sentinsi hii kwajinsi ilivyo katika lugha ya Kigriki inakuwa hivi ‘uje, ufalme wako, yatimizwe mapenzi yako!

Tunaweza tu kutangaza ukiri wa kinabii endapo tumesikiliza kile Baba yetu wa mbinguni anasema. Hili linakuja kutokana na uhusiano wa karibu na Mungu na usikivu kwa Roho Mtakatifu.

Mara tu unapoelewa yaliyo kwenye moyo na akili ya Mungu, unakuwa na mamlaka ya kutoa Tangazo la kinabii: unaweza kutangaza vitu hivyo na vikawa, kwa Jina la Yesu.


  1. Weka ukiri wako na Neno.

Ee Bwana, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele” (Zaburi 119:89)

Kama Yesu alivyodhihirisha, maneno ‘yaliyoandikwa’ yanaweza kuwa maneno yenye nguvu zaidi, yenye mamlaka na yanayotoa uhai tunapotamka. (Luka 4: 4) Neno la Mungu lina mamlaka na unapopata ufahamu wako juu ya kusudi la Mungu kwa Neno lake, ukiri wako wa kinabii unaweza kuwa na nguvu zaidi.


  1. Tambua kuwa ukiri wa kinabii unatokana na Nafasi yako, sio kanuni.

Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu” (Waefeso 2:6)

‘kuketi pamoja naye katika ulimwengu wa roho’ ina maanisha mamlaka ya kiroho na kiti cha enzi cha Mungu.

Kutangaza ukiri wa kinabii sio swala la kutamka maneno sahihiau kutumia kanuni. Unatokana na kile unachojua kuhusu ahadi za Mungu, kukutana na Mungu kwa mahusiano yako na Yeye – kutangaza kutokana na hayo.

Hivyo, Haijalishi kwamba utatumia maneno kuwa ninakiri, ninatangaza au kusema nina amuru. Hata ukitumia maneno ambayo Mungu alitumia kuumba dunia, mbingu na nyota – maneno yenye nguvu zaidi huku duniani – yalikuwa ‘na iwe’ (Mwanzo 1). Mamlaka haipo katika Kuongea – mamlaka ipokatika nafasi yako, kuketishwa pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu. (tazama pia Wakolosai 3:1-3)


  1. Tumia Jina la Yesu

Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mathayo 28:18)

Hatuwezi kudhihirisha mamlaka ya kifalme kwa majina yetu, lakini katika Jina la Yesu. Mamlaka yote ya Mbinguni na duniani amepewa Bwana Yesu na anatuweka sisi kwa mamlaka aliyopewa. Sisi tu warithi pamoja naye na Wawakilishi wake haa duniani, tukitangaza nia ya Baba yetu kwa wakati huu. Hivyo Unapotoa ukiri wakinabii hakikisha kuwa unatangaza kwa Jina la Yesu.


  1. Tazama kwa jicho la Imani

Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. 3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.” (Waebrania 11:1, 3)

Unapokuwa unatoa Tangazo la kinabii, koine kile unachokiri aukutangaza kikitimia kwa jicho la imani. Fahamu kuwa katika maneno yako Rasilimali za lifalme zinaachiliwa na mambo ya kidunia yakaa sawa.


  1. Tangaza ukiri wako

Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako.” (Ayubu 22:28)

Ukishakuwa na ufunuo wa kinabii kuhusu jambo lolote, unaweza kupatana na Mungu kuachilia kusudi lake. Hivyo songa mbele, tangaza na kukiri ukiri wa kinabii juu ya maisha yako katika Jina la Yesu subiri mpenyo unavyojitokeza katika maisha yako.

Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo. 20 Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.” (2 Wakorintho 1:19-20)


MUHIMU:

UKIRI NI AGIZO LENYE NGUVU YA SHERIA

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s