Alisema:

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

Matendo ya Mitume 1:8

Hajasema “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; na hiyo nguvu itwasaidia tu kunena kwa lugha au kuomba kwa lugha ya Roho Mtakatifu”.

Amesema, “hiyo nguvu itawawezesha kuwa mashahidi Wangu”

Nimekuwa Mtumishi wa Mungu kwa miaka kadhaa sasa – saba, nimekutana na watu wa aina nyingi lakini ukweli mpaka sasa ninaweza kusema nimewaona watu wachache sana huku duniani ambao ukweli wamepokea nguvu na ikatenda kazi vilivyo. Mungu anataka sisi tubatizwe kwa maji, tubatizwe kwa Roho Mtakatifu na tufikie kiwango cha zaidi ya kujazwa Roho Mtakatifu.

Ninaweza kukutajia mamilioni ya watu waliobarikiwa. Ninaweza kukuonesha mamilioni ya watu ambao wanahubiri Kuhusu Yesu. Ninaweza kukuonesha mamilioni ya watu ambao ukweli wananena kwa lugha mpya au watu ambao wanajisikia raha sana pale wanapomfanyia Mungu ibada.

Lakini bado sijakutana na watu ambao ninaweza kusema “kweli huyu anao uwezo uitwao nguvu, amejazwa Roho Mtakatifu, anatoa ushuhuda na ushahidi wa kufufuka kwa Yesu Kristo”. Tambua kuwa kutoa ushahidi wa Yesu Kristo ni kutoa uthibitisho kuwa Yesu alifufuka na ndiye Bwana.

Jambo hili nakuambia ndugu msomaji. Inawezekana kabisa kuwa na hiki kiungo muhimu cha injili kiitwacho NGUVU, ambacho kwa kiasi kikubwa kanisa la leo linakosa uzoefu wa nguvu za Mungu.  Lazima kwanza tuamini kwamba inawezekana na kuamua kuishi maisha ya njaa ya haki. Ila lazima hasi iwepo kabla ya kuzalisha nguvu.

Mafundi umeme wanasema ili kuzalisha nguvu ya umeme ambayo inaweza kufukuza giza na kuleta mwanga lazima ziwepo waya mbili.  Wanachukua waya ya hasi na chanya ndipo huweza kuziweka ndani ya ganda ili zisigusane isipokuwa mwishoni kila moja inaingia katika sehemu yake na mara nyingi wanachimbia chini. Lazima zisigusane Vinginevyo hazitafanya kazi au zitasababisha tatizo kubwa!

Mchakato wa kufikia nyaya au kuzitandaza chini si rahisi, Yesu alisema;

Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi”.

Yohana 12:24

Hii hatua siyo rahisi kabisa, ila ni ya muhimu sana kuzalisha nguvu. Maana ukiweka waya mmoja tu kwenye swichi, huwezi kupata umeme. Hupati hata mzunguko wa umeme, na hakuna mwanga wa kufukuza giza. Lazima uweke zote hasi na chanya pamoja.

Katika ulimwengu wa roho lazima ushughulikie mambo mabaya ili kwamba uweze kuzalisha mwanga tunaoutaka. Lazima uwe tayari kukabiliana na mambo jinsi yalivyo na wewe utakavyo. Tuna tatizo la watu kakata tamaa kushuhudia wengine kwa ajili ya Mungu. Kanisa linapoteza uwanja kwa sababu wasiookoka wanaongezeka kuliko kanisa.

Licha ya mtembeo wa Roho Mtakatifu katika mataifa mengi ya ulimwengu tunapoteza mechi. Watu wengi wa dunia hii bado hawajasikia habari za Yesu kwa ufasaha. Sijasema kwamba nusu ya watu walioko duniani wamemkataa Yesu. Sijasema labda wengi wamerudi nyuma. Ninachosema ni kwamba mabilioni ya watu bado hawajamsikia Yesu hata mara moja, hata kusikia jina la Yesu. Huu ni ukweli unaoumiza na uhalisia hatari sana.

Sababu kubwa ya hili ni kwamba wengi tumekwama mahali pa kutaka baraka zaidi na tumeshindwa kukazania kuwa na nguvu za Mungu ambazo zinahitajika ili tuweze kuzifanya kazi za Mungu. Narudia tena kusema kuwa mafanikio makubwa ya ufalme wa Mungu yatakuwa mikononi mwa wanaotafuta jibu la swali hili:

Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?”

Yohana 6:28

Watu waliojazwa Roho Mtakatifu, wapentekoste, wamezamia sana kwenye baraka, lakini Yesu hakusema “Mtapokea baraka…”

Alichosema Yesu ni kwamba: “Mtapokea NGUVU”

Kanisa limekwamia mahali pa baraka, kila kanisa utakaloenda wanaongelea baraka tu, kunena kwa lugha, mwanzo wa Uhusiano wetu na Roho Mtakatifu, tunakwamia hapo. Ni wachache sana ambao utakuta wanakazania kusimama kwenye wito, wengi wanahama. Ni wachache mno wanaingia na kudumu katika nguvu za Mungu.

Wengi wanapokea baraka zenye nguvu, lakini hawana vigezo vitakiwavyo kuweza kufukuza mapepo. Hawana vionjo vinavyotakiwa kuponya wagonjwa. Na hii ndiyo kazi ambayo Yesu aliagiza tuifanye.

Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya”

Marko 16:17-18.

Jibu ni lipi? Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?

Ili kuzifanya kazi za Mungu lazima tuwe tayari kwenda katika viwango zaidi ya tulivyo navyo. Tusikwamie tu kwenye kiwango cha baraka katika maisha yetu. Lazima tupenye katika ulimwengu wa roho ili tuingie katika ulimwengu wa roho wa nguvu za Mungu.

Kwa neema YA Mungu tutafikia viwango hivyo mpaka tunapofika mwisho wa mfululizo wa somo hili.

🗣 OMBA:

  1. Omba Mungu, akupe neema ya kuvuka viwango vya baraka na kufikia nguvu za Mungu ipasavyo, katika Jina la Yesu Kristo. Amina!

Unaweza kujiunga kwenye group la Goodvine Discipleship School la WHATSAPP kwa kujaza fomu hapa chini:

http://forms.gle/957djapjw8gFLkF36

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s