TAMANI SANA NGUVU KULIKO BARAKA

Mafanikio makubwa ya Ufalme wa Mungu kwa siku za badaye yatakuwa mikononi wa wale tu wanaotafuta jibu la swali hili:

Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?

Yohana 6:28

Kanisa la Bwana Yesu limeomba kwa miaka na miaka juu ya kutamani kumuona Mungu kwa kiwango cha juu sana. Na ili kufanikisha hilo wamefanya mikutano mingi ya uamsho, kufunga, mikutano ya hadhara, Matangazo, ushirika, ushirika. Zamani watu walibarikiwa sana, walifurahia uwepo wa Mungu, walicheza katika roho, zilikuwa nyakati kubwa za furaha na baraka.

Tatizo ni kwamba kanisa, mwaka hadi mwaka hadi mwaka, limekwama kwenye baraka tu, na haliingii tena katika uhusiano wa kiroho ambao Mungu ameukusudia! Hatujafika mahali panapotahili. Swali kubwa ni kwa umbali gani unatamani kufika?

Tuna majumba mazuri, mavazi mazuri, tuna misalaba mizuri, tuna madirisha mazuri ya udongo. Tuna kwaya nzuri zenye nyimbo nzuri, tuna ushirika na vyakula vizuri. Tuna watu madhababhuni ambao wameenda seminari kusomea theolojia au wamechukua kozi ya miaka mitatu mpaka minne na wanajua maana ya ibada. Wana uwezo wa kufundisha pointi kwa pointi.

Wanabatiza watoto, wanafungisha ndoa watoto wakikua, wanasikiliza matatizo yao, wanawafuta machozi, wanazika waliokufa. Lakini kuna jambo la msingi sana tena linalohitajika sana! Hayo yote hayatoshi.

HALI HALISI

Jambo ambalo ninakushirikisha leo ni hali halisi ndiyo hali halisi la kanisa la leo.  Hakuna anayependa kujifunza au kusikia mambo mabaya ila ili tuweze kujifunza namna ya kutenda kazi za Mungu, lazima tuyakabili mambo kama yalivyo na si kama sisi tunavyotaka yawe. Lazima tuongee Ukweli hata kama unauma na hata kama unapingana kabisa na kile ambacho tulikiamini maisha yetu yote.

Ni hivi:

Mafanikio yote yanatokana na kujishughulisha na watu, mahali, vitu kama vilivyo na siyo ambayo wewe ungetamani vitu viwe. Kwa kifupi naweza kusema mafanikio ni kushughulika na watu kam walivyo, siyo kama wewe ulivyo.

Hivyo, lazima pia tushughulie hali zote kama zilivyo: Biblia inasema kuwa:

“tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”

Yohana 8:32

UKWELI NI HUU!

Ukweli ni kwamba Kuhusu hali halisi ya kanisa, watumishi na waamini wa siku za leo tupo kwenye tatizo. Na tatizo lenyewe ni kukata tamaa! Yesu alifufuka miaka 2000 iliyopita lakini leo kuna mabilioni ya watu hawamjui Yesu. Hatutaweza kuliondoa tatizo hili kwa kulipuuzia au kusema halipo. Huu ni wakati wa kujipanga na kuzama katika Neno la Mungu ili tuweze kujua hasa mapenzi yake na kusimama imara kama ahadi zake zilivyo kwetu. Lazima tutafute ufunuo mpya, mpenyo mpya ambao utatuingiza katika kusudi la ulimwengu wa roho zaidi ya hali ya sasa.

Hali ya sasa ni ya kushangaza sana, utaona mtu anasema ameokoka bado anakunywa pombe, anasema ameokoka bado mwongo, bado ana mke au mme nje ya ndoa, anasema ameokoka lakini hawezi kujitoa kwa ajli ya kazi ya Mungu. Anasema ameokoka lakini hana hata uwezo wa kumaliza mchawi, magonjwa kila siku ndani yake, umaskini wa kutosha, na woga mwingi. Na mbaya kuna baadhi ya watumishi wanapenda zaidi pesa kuliko kumtafuta ahadi ya Bwana Yesu kwa kanisa.

Kanisa limekosa kweli kubwa sana ambayo Bwana Yesu alifundisha mara zote. Wanalijua Neno, wanauwezo wa kukalili moyoni, lakini wamekosa Ukweli hali wa hilo Neno, kile ambacho Neno linaweza kufanya na Roho Mtakatifu na hili ndilo limekuwa “bomu” la kiroho.

Ni wazi katika Neno, Bwana amekusudia kwamba kanisa liwe na nguvu ya Roho Mtakatifu ili kuweza kuufikia ulimwengu, lakini kanisa limekosa hii nguvu tena pakubwa.

Yesu alipotuahidi kwamba tutapokea Roho Mtakatifu, hajawahikutuahidi kwamba tutanena kwa lugha tu. Zoea kuwa na nguvu! Nenda zaidi ya kiwango cha baraka na uingie katika kiwango hatma ya kinabii ya Mungu kwa ajili ya kania lake. Kuna zaidi ya katika Pentekoste kuliko kushika elimu tu. Kuna kuzeoa Nguvu. Maana ukizoea kuwa na Mungu utashinda hata ukikutana na Farao na ukatoa tamko “Bwana wa Isareli aseme, ruhusu watu wangu waende!”.

Tunatakiwa kuwa na kiu hasa ya kuwa na nguvu za Mungu kuliko hata unavyotamani kubarikiwa. Yesu hakuwaambia wanafunzi wake wasubiri pale Yerusalemu mpaka wapokee baraka, au kipiwa cha kunena kwa lugha. Aliwaambia:

“…mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu…”

Matendo ya Mitume 1:8

Walikuwa wanangoja NGUVU ya Roho Mtakatifu! Siku za leo watu wamekuwa wavivu sana kungoja mbele za Bwana. Wengi wamekwama kabisa kuvuka kiwango cha kutamani baraka na kufikia Ahadi ya Bwana Yesu. Ahadi ya Bwana Yesu ni NGUVU.                                                                                                    

🗣 OMBA:

  1. Omba Mungu akupe neema ya kujiliwa na nguvu ya Mungu ili uweze kuleta maana katika ufalme wa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo. Amina!

Unaweza kujiunga kwenye group la Goodvine Discipleship School la WHATSAPP kwa kujaza fomu hapa chini:

http://forms.gle/957djapjw8gFLkF36 AU Tuma meseji kwenye namba 0752122744 Ikiwa na jina lako na mkoa unaoishi.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s