Mtendaji wa Neno ni muujiza na kila walichonacho ni muujiza. Mtendaji wa Neno, ndiye Mtunza amani, sio viongozi wa ulimwengu waletao amani bali wajuao Neno, kwa sababu mfalme wa amani anaishi ndani yao. Hivyo popote awapo husababisha utulivu na ukiona ulipo unasababisha vurugu jua mfalme wa amani hayupo.

 • Mtendaji Neno hawezi kumruhusu Yesu alale, maana ameingia ndani ya merikebu yake.
 • Neno linasema “ninyi wenye kumuamsha Mungu msimwache apumzike”
 • Acha uzoefu, maana Petro alijaribu kutumia uzoefu wake wa kuvua samaki kwenye maji lakini hakuweza kuituiza dhoruba – wakamwambia Yesu wewe huoni tatizo?
 • Mtendaji wa Neno hapungukiwi na chochote kwa sababu Neno linazalisha chochote kwa ajili yao. Yohana 1:1-5
 • Neno linatabia ya kwenda pale linapokaribishwa na kuondoka mahali ambapo limekataliwa. Mungu alimwambia Yoshua katika Yoshua 1:8
 • Unalikataaje Neno? Ni pale unapojidharau mwenyewe. Neno huliwezi kukaa kwa anayejidharau

MAMBO MANNE YA MSINGI KATIKA NENO

 1. SIKIA NENO:Unaweza kusikia Neno kwa kusoma, kusikiliza toka mwalimu, CD, vinasa sauti n.k. Ukisikia unabaini kipi sawa na kipi si sawa.
 2. ONGEA NENO: Maana yake sema ukweli Kuhusu wewe usiseme uongo, hata kama ulikosea wewe sema Ukweli. Na kweli itakuweka huru, wengi weno kweli haimo ndani yako – na hii ndiyo sababu hamfanya mambo makuu. Siku utakapoelewa Neno, utaanza kusema na kweli na Baba wa Mbinguni atakupenda zaidi.
 1. TENDA NENO.
 2. UWE NENO: Acha kujifanya unaweza, Ruhusu Roho wa Mungu achukue nafasi ndani yako ili akufanye mtendaji. Ukiwa msomaji, msemaji, mtendaji wa Nenoo kamwe hutakuwa chini, maana Neno limetoka juu na daima litakupeleka juu, hivyo ukiwa Neno kamwe hutakuwa Neno.

UTAJUAJE KAMA SASA UMEMPAta mungu / neno?

1.  Unakuwa mzalishaji

2.  Hutikiswi

3.  Kila utendalo litafanikiwa: ndani yake hakuna huzuni, uchungu, upweke, ndani yake hakuna utasa – ni chanzo cha kila kitu kizuri na kibaya. Ukiona unayo hayo jua Yeye hayupo – yaani Neno halipo.

TANGAZA KUWA: –

 1. Mimi ni Nuru na daima nitawaangazia wengine
 2. Nitasikia, nitaongea na nitanda Neno ili niwe Neno.
 3. Msamiati wa kushindwa sio wangu kabisa. Msamiati wangu ni huu “NAWEZA” Msamiati wangu ni “INAWEZEKANA” Ndiyo maana Biblia inasema yote yawezekana kwake yeye aaminiye.
 4. Watu wa kanisani na watu wengine watakopa toka kwangu.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s