Mungu anawapenda wanadamu na wanadamu wanampenda Mungu. Hivyo, Mungu na wanadamu wanapendana, kila mmoja anampenda mwenzake kwa wakati wake, Mungu alishafanya vitu kadhaa vinavyoonesha kuwa alishachukua hatua ya kuwatafuta wanadamu. Kuna wakati tunaona upendo wa Mungu pamoja na Adamu. Lakini pia tunaona Mungu anavyomtokea Musa ili awakomboe wana wa Israeli. Mungu mara kadhaa amewatoa watu wake mikononi mwa maadui.

Kubwa ni hili la kumwaga damu ya mwanaye Yesu Kristo ili atukomboe, Yesu mwenyewe akasema “Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” – Luka 19:10. Pia Mtume Paulo akasema “Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi” – 1 Yohana 3:8. Kuna wakati Mungu anampata mtu wake na kumuonesha njia ya kupita, japo kuna wakati hawa watu wanapoteza uwepo wa Mungu na anauliza umegeukaje na kuwa mzabibu mwitu? Yeremia 2:21.

Kwa neema, inatokea tena wanadamu wanaanza kumtafuta Mungu, na kwa yeyeote anayemtafuta Bwana anampata, ndiyo maana Yeye amesema

ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao

2 Mambo ya Nyakati 7:14

Hii inaonesha kuwa Mungu anaondoa uwepo wake kwa watu ambao wanaacha maagizo au njia ya Bwana. Na kama kuna kitu cha muhimu sana kwetu ni kuwa na uwepo wa Mungu. Maana ukiwa na uwepo wa Mungu hakuna ugonjwa, uchawi au nguvu za giza zinazoweza kukuangamiza. Hata ibilisi hawezi kumwangamiza mtu mpaka kwanza Mungu aondoe uwepo wake kwa huyo mtu (Ayubu 1:6-12).

Mungu anapatikana kwa wale wamtafutao, na hao wamtafutao wanaweza kumtafuta kwa kusoma Neno la Mungu, kuomba na kufunga. Unaposoma Neno hakikisha unamuomba Roho Mtakatifu akufunulie siri ya lile Neno maana Roho ndiye aliyeandika hilo Neno kupitia Mwandishi. Hivyo mtu anaposoma Neno la Mungu lazima umulize Roho Mtakatifu una maana gani katika hiki nisomacho? Njia ya piliyakumtafuta Mungu ni kuomba pamoja na kufunga.

SABABU KUU TATU ZA KUFUNGA NA KUOMBA:

“Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. 10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.”

1 Mambo ya Nyakati 4:9-10

Yabesi akamlingana Mungu, hii inaonesha kwamba aliomba kwa Mungu na inawezekana maombi yake yaliambatana na kufunga ili Mungu aingilie kati ile hali yake ya huzuni. Uwepo wa Mungu ukiwepo hatuhitaji kufunga maana yupo mwenyewe (Marko 2:19). Huwezi ukafunga wakati Mungu yupo na wewe tunafunga ili kumtafuta aje atuzinguke na uwepo wake.

Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana? 6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?

Isaya 58:4-6

Tunabaini haraka tu kuwa mfungo

 1. TUNATAKIWA KUFUNGA ILI TUJITAMBUE SISI KUWA NI WANADAMU: Maana inawezekana kama mwanadamu angekuwa na uwezo wa kufanya kila kitu bila kufunga lazima angeweza kujifananisha na Mungu. Kuna vitu huwezi kuvipata mpaka unyenyekee kwa kulia na kutoa machozi, tujitambue kuwa sisi tu wategemezi na hatuwezi bila msaada wa Mungu.
 1. TUNAFUNGA KWA SABABU YA KUNYENYEKEA: Tunafunga ili kuonesha unyenyekevu kwa Mungu, ambayeanajibu maombi yetu kwa ajili ya maisha yetu.
 1. KUFUNGA NI ISHARA YA KIU YA KUPOKEA KITU TOKA MUNGU: Tunasema tunapofunga, kumtafuta Mungu ni muhimu sana kuliko kumtafuta chakula. Kufunga kuna maanisha kuwa sisi tuna kiu na Mungu kuliko kkitu kingine chochote.

Acha niseme tena kuwa: maombi kwa mungu pamoja huachilia mpenyo wa nguvu za kiroho.

Ninamalizia kwa kusema mambo kadhaa ya kuangalia unapokuwa unafunga na kuomba:

 1. Mfungo lazima usiwe “wa kinafiki” (tazama Mathayo 6:16).
 2. Mfungo lazima uwe siri (Mathayo 6:18)
 3. Kufunga katika Biblia daima kunaambatana na maombi.

Yesu Akawaambia, Muda wote walipo na bwana-arusi (akijizungumzia mwenyewe) pamoja nao hawawezi kufunga. Hivyo alisema “Watafunga”. Tunahitaji nguvu sana maishani mwetu, katika kanisa, familia zetu n.k. ninaamini kwamba Yesu alikuwa anamaanisha sisi tufunge na kuomba. Kama unaona ukame wa kiroho, unapokosa nguvu ya kuushinda ulimwengu? Je unahitaji kuhuishwa? FUNGA na KUOMBA.

🗣 OMBA:

 1. Tuombe Roho Mtakatifu atuongoze katika maombi ya mwezi huu ili tuombe sawasawa na mapenzi ya Mungu yale yaliyo moyoni mwake.
  1. Roho wa Neema na maombi awe juu ya kila mtu.
  2. Mruhusu afurike ndani yako jitiishe chini ya uongozi wake.
  3. Omba kibali cha kusikilizwa maombi yetu ili tusiombe kwa hasara bali kwa faida.

Unaweza kujiunga kwenye group la PASTORBON WHATSAPP kwa kujaza fomu hapa chini: http://forms.gle/957djapjw8gFLkF36

One thought on “NGUVU YA KUOMBA PAMOJA NA KUFUNGA

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s