“Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao.”

Zaburi 147:3

Agano jipya limejaa matukio mengi ya watu ambao waliponywa, lengo kubwa ni kutushawishi sisi kwamba uponyaji unawezekana kupitia Yesu Kristo. Zipo fadhila, utukufu na nguvu ya ajabu sana ndani ya jina la Yesu. Kila aliyewahi kukutana na Jina hili au Nafsi yake hakuwahi kubaki alivyokuwa, haijalishi ukubwa au udogo wa kiwango cha ugonjwa waliokuwa nao. Kila kitu kinawezekana kupitia Jina la Yesu. Tunasoma;

akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye

Kutoka15:26

“Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana”.

Mathayo 19:26

Kupitia Jina la Yesu kuna nguvu kubwa sana ya kushinda kila aina ya maradhi na magonjwa.

“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;-

Wafilipi 2:9-10

Endapo utatambua kuwa Yesu alilipa gharama zote kwa ajili ya ukombozi wetu ili tuwe huru dhidi ya kila magonjwa, ndipo utaweza kukubali kwa ujasiri kuwa Bwana Yesu ndiye chanzo cha uzima wetu. Kupitia wokovu Bwana Yesu ametupatia; uzima, afya, amani na vingine vingi kwa wingi. Yeye mwenyewe alichukua maumivu yetu na akabeba magonjwa yetu. Mara zote anatamani kufanya vitu ili kulithibitisha Neno lake, na ili tutambue kipimo cha mawazo ya Mungu juu yetu.

Kama unauhitaji wa muujiza mmoja wa uponyaji au jambo linguine, au umeteseka na maumivu ya magonjwakwa muda mrefu, Bwana Yesu atadhihirisha ukamilifu wa utakaso na nguvu ya uponyaji katika maisha yako. Unachohitaji ni kuwa ina Imani kwake tu. Petro na Yohana walikuwa hawana msaada na hawakuwa na elimu,lakini ukweli unabaki palepale kwamba walikuwa na Yesu na walitambua kwa vitendo kwamba jina la Yesu lina uweza kutenda maajabu. Walimuambia mtu katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri kusimama na kuondoka, na yule bwana akapokea uponyaji wake mara moja.

Kuna mtu anasoma ujumbe huu wakati huu, haijalishi umekosa msaada kiasi gani au umepoteza matumaini kiasi gani, hata kama ripoti ya madaktari ni mbaya kiasi gani, Bwana wangu, Yesu Kristo atabadilisha habari zako katika Jina la Yesu. Kupitia jina la Yesu magonjwa yasiyo na tiba yanatibika. Kupitia jina la Yesu, viwete watatembea na vipofu wataona. Kupitia Jina la Yesu wenye ukoma wanatakasika kimaajabu. Katika hii dunia yetu, ambapo magonjwa mapya yanaibuka kila sikuna yanawachanganya madaktari hata hawana ufumbuzi wakudumu au hata kuyatambua wanashindwa, unahitaji sana umtegemea huyu Daktari Mkuu – Bwana Yesu. Anao uwezo wa kuponya kila aliyevunjika moyo na kuharibu kila nguvu za kishetani. Kwa kuwa na Imani katika Jina lake na damu yake, uponyaj na ukombozi vinakuwa ni matukio ya kila siku.

watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya

Marko 16:18

“Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye”.

Yeremia 30:17

Kwa neema kuu ya Mungu, Yesu amekuwa daktari tangu nimekuja kufahamu kweli hii. Hii ndiyo sababu kila mara ninapopata nafasi ya kuwa hudumia watu, ninafuata tu maelekezo ya daktari wangu mwaminifu, na kumruhu ajitukuze mwenyewe. Sijawahi kuhangaika kwamba sijui uponyaji utatokeaje, mimi nanichofanya ni vile tu anavyoniamuru.

Moja ya chanzo kikubwa cha magonjwa ni dhambi. Kama unaishi maisha mabayo yanamfurahisha Mungu, magonjwa kamwe hayatapata nafasi mwilini mwako. Haijalishi watu wangapi wanapata magonjwakaribu na wewe, ahadi ya Mungu ya kuwaweka salama wana (watoto) wake dhidi ya magonjwa yanayowapata wengie iko palepale. Kama unaruhusu dhambi maishani mwako tambua kabisa kuwa utakuwa unatuma mwaliko kwa magonjwa kwa sababu dhambi na magonjwa vina uhusiano mkubwa. Tubu leo na ufuate njia ya uzima. Tunaporudi kwa Bwana, mataifa yetu pia yanaponyeka na jamii zetu pia zinaponyeka na hata magonjwa yanakuwa hayana nafasi kwao.

MAOMBI na wimbo wa kusikiliza kabla ya maombi

Chanzo cha Uzima (Anna Komba)
  1. Mtukuze Bwana kwa maneno ya kinywa chako au nyimbo.
  2. Mwambie Bwana naomba unisamehe dhambi zangu (Taja unazokumbuka)
  3. Baba, kwa jina la Yesu Kristo, naomba uniponye kila aina ya ugonjwa na maradhi.
  4. Baba, kwa Jina la Yesu, naomba unibatize kwa Roho Mtakatifu na moto wako ili kamwe nisikutane na magonjwa au maradhi tena.
  5. Baba, kuanzia leo ruhusu uponyaji wako uanze maishani mwangu.
  6. Baba, kwa Jina la Yesu naomba uwaguse ndugu zangu, marafiki (taja majina yao) na uwafanye wawe na afya njema.

4 thoughts on “BWANA ATAKURUDISHIA AFYA

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s