Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanyama na binadamu. Kwa binadamu, jamii kadhaa za virusi vya Corona vinafahamika kusababisha maambukizi kwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji.  Maradhi yaliyowahi kusababisha madhara makubwa kutokana na virusi vya Corona ni pamoja na MERS na SARS yaliyozuka mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kirusi cha Corona kilichogundulika hivi karibuni kinasababisha ugonjwa unaofahamika kama COVID-19. COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya havikuwa vikifahamika hapo kabla na sayansi ya tiba. Na vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.

Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.

ISAYA 26:20

Neno la Mungu linatuongoza kufanya mambo ambayo ni kwa usalama wetu tulio watu wake Mungu. Inasasikitisha sana kuona kuna watu hawataki kufuata utaratibu unaotolewa na serikali ili kujikinga na janga hili hatari linaloitesa dunia. Neno hapo juu ni agizo kwetu hasa inapotokea Mungu anataka kushughulika na watu fulani, anasema njooni watu wangu:-

  1. Ingia ndani kwako: Tunapoambiwa tutulie nyumbani na viongozi wa serikali sio kwamba labda wametumia akili zao, hapana! Ni utaratibu wa Mungu kuwahifadhi watu wake ndani wakati anataka kuwapiga waovu. Sasa akikuta unazungukazunguka bila sababu anakujumlisha pamoja nao.
  2. Funga mlango: Wanafunzi na wazazi wa wanafunzi shule zimefunga ili familia zifungiwe ndani ya nyumba. Tafadhari punguzeni safari za kutembelea ndugu na kudhurula mitaani. Ni rahisi kukutana na maambukizi kwa kukosa utii wa agizo.
  3. Jifiche kidogo: Kumbe Mungu anakupenda kiasi hiki hata ataka uweze kutulia ndani ili usije pigwa pamoja na wanaotakiwa kupigwa. Ni muda wa kuomba sana ili kukusanya nguvu ya Mungu kwa ajili ya kuitumia pale ambapo itakuwa tayari ghadhabu hii itakuwa imepita.

Watu wengi, hasa waaminio wanaona kama maamuzi ya serikali ya kuzuia mikusanyiko ya watu, kufunga shule, kufunga mipaka na safari za ndege wanaona kama ni mambo ya kidunia na wakii hili watakuwa hawajatii imani yao kwa Mungu, hili sio sawa kabisa. Ninatamani tutambue kuwa kuna magonjwa ambayo yanakuja kwa sababu Mungu amechoshwa na tabia za watu wake aliowaumba, mfano kuna nchi zinaruhusu utoaji mimba, kuna nchi zinaruhusu ndoa za jinsia moja na kuna nchi zinanyanyasa nchi nyingine, lakini pia kuna tabia za ushoga, ufisadi, uzinzi, mauaji n.k hivi vyote vinapozidi zinamfanya Mungu alete ghadhabu duniani, na hi inaweza kuanzia taifa moja kwenda jingine kama alivyosema;

32 Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia. 33 Na waliouawa na Bwana siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi.

YEREMIA 25:32-33

Uovu unaotokea toka taifa hata taifa ndiyo chanzo kikubwa cha magonjwa ya mlipuko, haijalishi watasema ametengeneza mtu au ndege au panya, wewe tambua kuwa Mungu ameruhusu hilo litokee kwa sababu hajapewa heshima anayostahili. Ndipo huinua tufani (mfano wake ni hii korona au COVID-19). Unashuhudia kabisa au kusikia hata wanaokufa kila upande wa ndunia hi hawaliliwi yaani hakuna mkusanyiko wa misiba yao, wengine hata ndugu hawagusi wanazikwa naserikali na unakuta ndugu wanaishia kuzika kwa taarifa lakini hawaendi msibani.

Mimi na mke wangu Vaileth, tunawaomba ndugu wasomaji, tulieni nyumbani na kama unaenda kazini fuata taratibu zote za kukusaidia kuwa salama. Kuambiwa utulie nyumbani ni agizo la kiungu kabisa na kwa kufanya hivi niseme tu serikali za dunia hii zimemsikia Mungu hata kutoa maagizo haya.

NI SEHEMU GANI HATARISHI ZAIDI KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA KORONA?

Sehemu za kuepuka kabisa

Sehemu za starehe kama vilabu na baa, migahawa, nyumba za mazoezi, saluni, sehemu za kuangalia michezo, majumba ya sinema, mikusanyiko ya hadhara na sherehe

Sehemu ambazo inaweza kukulazimu kwenda

Kuwa makini sana ikikulazimu kwenda sehemu hizi: Vituo vya basi, nyumba za ibada, hospitali, usafiri wa umma, benki, madukani na masokoni

Sehemu salama

Nyumbani kwako na ndani ya gari binafsi lakini kumbuka kuwa usalama huu hupungua unapoalika wageni au kuwapa watu lifti

Vitu vya kutumia kwa tahadhari

Sarafu na Noti, kuta na milango ya sehemu za umma, sehemu za pembeni ya ngazi, sehemu za kushikilia kwenye daladala, milango ya usafiri wa umma, vifaa tunavyotumia mara kwa mara kama simu, bakora au magongo ya watu wenye ulemavu.

Kwanini watu wanawekwa karantini?

Kwa ufupi neno Karantini linamaanisha kuwa chini ya uangalizi. Watu wenye dalili au wanaotokea maeneo yenye maambukizi makubwa ya virusi vya Corona hulazimikwa kuwekwa karantini (kutengwa na watu wengine) ili kufuatilia afya yao kwa karibu na kuzuia kueneza virusi. Ukiambiwa unapaswa kuwekwa Karantini, usiogope. Ni kwa ajili ya afya yako na wengine. Mungu mwenywe.

3 thoughts on “FUATA UTARATIBU KORONA INAZUILIKA

  1. Amina baba Mungu akubariki, akupe uwezesho Mimi binafsi nabarikiwa sana na mafundisho yako.

    Emmanuel.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s