Dunia yetu ipo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo. Maadui wetu sasa sio wanadamu tena bali ni wale ambao hata hatuwezi kuwaona ingawaje wakati mwingine wanaishi ndani yetu. Tunahitaji kitu kikubwa sana kuweza kushinda vita tunayopambana na adui yetu, tunahitaji nguvu ya Mungu.

siku ya uponyaji na ukombozi wa taifa la Tanzania

Kwa sababu ya hili lazima tufanye kwamba kuombea taifa liwe jambo la kuzoea, siyo kusubiri matukio mabaya yatupate. Biblia inasema;

Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.

Ufunuo wa Yohana 5:8

Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika.

Ufunuo wa Yohana 8:4

Hii ina maanisha kwamba tunapoomba maombi yetu yanakusanywa nahayatupwi, yanadumu. Hatuombi na hayo maombi yakaishia hewani. Mombi yetu yanaongezeka hivyo, hatuna budi kujaza vikapu vyetu. Lazima tuzidi kusongea kwenye wito mkuu wa Mungu kwa maombi ili ufike wakati maombi yaamue tuishi badala ya kifo, tushinde badala ya kushindwa. Yesu alisema;

Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa.

Luka 18:1

Mungu ametuita mimi na wewe tuwe vyombo vyake vya uponyaji, upendo, ukombozi na wokovu, si tu kwa taifa letu bali pia kwa mataifa mengine na dunia nzima. Amesema;

angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.

Yeremia 1:10

Kwa kadri tunavyoungana kwa ajili ya maombi kitaifa, tunakumbushwa kuwa “kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu (Luka 1:37).” hii inatuahidi kuwa hakuna jambo ambalo Mungu haliwezi. Tunapoamua kuomba kama taifa chini ya Mungu, sisi tunakuwa wakubwa kuliko janga linalotukabili. Kupitia maombi tutashinda vita hii kwa msaada wa Mungu na tutakuwa imara kuliko siku za nyuma na taifa letu litapokea baraka na umoja toka kwako.

MAOMBI

 1. Baba, tunakushukuru kwa upya kwa uwepo wako na kwa jinsi unavyojidhihirisha katika taifa letu la Tanzania. Neno lako linasema: (Zaburi 105:1 “Haleluya. Mshukuruni Bwana,liitieni jina ,Wajulisheni watu matendo yake“).
 2. Baba, kwa jina la Yesu Kristo tunaomba rehema zako na pia tupate neema ya kulihesabia haki taifa letu la Tanzania katikati ya janga hili la korona (COVID-19). Yoeli 2:13 rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya:
 3. Baba, kwa Jina la Yesu Kristo, tunang’oa kila uovu, na chukizo lilipondwa kwenye taifa letu la Tanzania. (Mhubiri 3:2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;)
 4. Baba kwa mamlaka ya jina la Yesu, tunang’oa kila mizizi ya magonjwa ya tauni (COVID-19) kwa kuwa huu. Na tunaomba umimine damu ya Yesu Kristo kwa ajili ya upatanisho wa taifa letu na WEWE BWANA. Hesabu 16:46-48 “Musa akamwambia Haruni, Haya, shika chetezo chako, ukatie moto ndani yake, moto wa madhabahuni, kisha utie na uvumba juu ya moto, ukakichukue haraka, wende nacho katika huo mkutano, ukawafanyie upatanisho; kwa kuwa ghadhabu zimetoka kwa Bwana; hiyo tauni imeanza. 47 Basi Haruni akakishika chetezo kama Musa alivyonena, akapiga mbio akaenda katikati ya mkutano; na tazama, tauni ilikuwa imeanza kati ya watu; akatia uvumba juu ya moto na kufanya upatanisho kwa ajili ya hao watu. 48 Akasimama kati ya hao waliokufa na hao waliokuwa wakali hai; tauni ikazuiwa)
 5. Baba, kwa jina la Yesu tunabomoa kila aina ya kiambaza kilichotutenga na Mungu wetu, na kazi za ibilisi zilizofanikisha kuingiza tauni katika taifa letu. Iwe ni tabia, au roho chafu, pepo wabaya na kila aina ya mawakala wa ibilisi wa kueneza magonjwa (Waefeso 2:14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga).
 6. Tunabomoa kila elimu za adui zilizopenya ikulu, mahakamani, bungeni, katika ofisi za serikali na makanisani, kwenye elimu yetu, uchumi wetu, kwa waalimu na wanafunzi ndani ya taifa letu na kusababisha hasira ya Mungu juu yetu, maana umesema “Isaya 54:13 Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.
 7. Ee Baba, kwa Jina la Yesu, tunaharibu kazi za ufalme wa giza ndani ya taifa letu na kila roho za magonjwa hasa huu ugonjwa wa korona unaolitesa taifa lako wakati huu, Ruhusu moto wa Roho Mtakatifu kuunguza kila kazi za uovu ndani ya nchi yetu ya Tanzania. “Yeremia 51:20 Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;
 8. Baba tunaangamiza kila kazi za ibilisi zinazopinga kweli ya Neno lako ndani ya taifa letu. Kila chombo cha habari ambacho kinafanya kazi ya kutoa taarifa za uongo, uchochezi wa kila aina Bwana tunakiangamiza. Kila chombo chenye ajenda ya siri ya kubomoa taifa letu tunakiangamiza leo, kwa Jina la Yesu. “Isaya 32:7 Tena vyombo vyake ayari ni vibaya; hutunga hila mbaya, ili kuwaangamiza wanyonge kwa maneno ya uongo, mtu mhitaji ajaposema maneno yenye haki.
 9. Baba, kwa Jina la Yesu tunakusihi ulijenge taifa letu katika msingi wa Neno lako, kuanzia ikulu, mahakama, na bunge vifanye maamuzi kwa mashauri ya Neno. Jeshi letu lijenge na liimarishe liwe na nguvu na ujuzi wa hali ya juu katika utendaji wake. Tunaomba ulijenge taifa letu la Tanzania likujue Wewe, katika msingi wa imani kwako, ujasiri, na uboara wa akili ili tufanye, mambo makuu. “Warumi 8:31… Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?“.
 10. Baba yetu uliye juu mbinguni, kwa Jina la Yesu tunaomba uridhie taifa letu liongozwe na Roho Mtakatifu nyakati zote kwa kila kiongozi aliyepewa mamlaka ili viongozi wa kitaifa waweze kuongoza watu kwa kutusogeza karibu na wewe Mungu unayeishi, ili taifa hili liwe taifa lenye hofu kubwa ya Mungu. “Yohana16:13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake“.
 11. Baba, Neno lako linasema wewe ndiye “utoaye nguvu za kupata utajiri. Kumbukumbu la Torati 8:18” na umesema “Mithali 10:22 baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo“. Kwa namna hii tunaomba uinue uchumi wa taifa letu na kila Mtanzania, ufanye uwe mkubwa na imara, kwa jina la Yesu.
 12. Baba, kwa jina la Bwana Yesu, tunaomba Jina lako na sheria zako ziweze kuinuliwa katika mashule na vyuo vyote vya nchi hii. Tunatambua kuwa ni wewe Bwana umekusudia elimu itolewe kupitia roho wako wa ufahamu na maarifa. Inua vijana wenye hofu kubwa ya Mungu ambao watasababisha taifa hili liinuke sana.
 13. Baba, kwa jina la Yesu tunaomba ulilinde taifa hili dhidi ya kila adui. Linda mipaka yetu na utuzunguke tusijevamiwa na yeyote. Tunaomba asiwepo adui ambaye atainuka kinyume chetu asifanikiwe. Pia tunaomba usalama wa ndege zinazoingia na kutoka katika nchi yetu, viwanja vyetu vya ndege, kila mipango mibaya isifanikiwe. Tunaomba kwamba kama taifa, na Watanzania wote tutaishi katika amani, tutalala na kuamka katika wewe, tufanye tuishi katika usalama wako. Zaburi 4:8 “Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.”

NENO LA BWANA KWA TANZANIA

1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. 2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. 3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. 4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao. 5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, 6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri, 7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe. 8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki. 9 Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. 10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako. 11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. 12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu. 14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. 15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; 16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.

ZABURI 91:1-16.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s