Taifa ni la Mungu na watu wakaao katika taifa hilo ni wa Mungu, hakuna watu wa mtu bali ni wa Mungu. Serikali za wanadamu zinapata kibali toka Mungu. Serikali ya aina yoyote inapata kibali toka Mungu. Kanisa ni serikali ya Mungu, ni sehemu ya wajumbe toka Mungu; wanazungumza na kusema ya Mungu kwa watu wa duniani.

Maombi ya kuombe nchi na Rais wa nchi yetu.

Katika jamii za wanadamu duniani Wafalme, Maraisi au mawaziri wakuu wanaoongoza Nchi hizo wanapata kibali toka kwa jamii husika, kwa wananchi husika; kupitia kura au kwa jinsi yoyote wanayopata; lakini wanapata kibali toka kwa Raia wake. Katika yote Mungu anahusika kwa sababu hao watu ni wa Mungu, akiona unafanya vizuri ana kuneemesha, ukifanya vibaya anakubadilisha au anakuondoa.

Nimehimizwa kuliambia taifa kwamba Watumishi wa Mungu waliopo katika Nchi hii kama kuna siku waliwahi kuomba basi ni sasa. Kipindi hiki ni kipindi muhimu sana kwa watumishi waliotwa kwa jina lake Mungu kuomba kwa bidii katika maeneo yote walioko.

Mambo ya kuZINGATIA KATIKA MAOMBI

1. KUIOMBEA NCHI YA TANZANIA NA WATU WAKE: Tuiombee Tanzania kwa sababu hali sio nzuri; Ulimwengu unapita kwenye misukosuko mingi wanahitaji watu walioitwa kwa jina la Mungu waweze kusimama kuliombea taifa; hasa taifa la Tanzania, ili waweze kuwa salama na waweze kulindwa na Mungu na Majanga yanayopita.

2. KUOMBEA RAISI WA TANZANIA, WASHAURI WAKE NA SERIKALI YAKE: Kama kuna kipindi Watanzania wanahitaji Kumuinua Raisi wa Nchi ni sasa; hasa ukilinganisha na yale ambayo anayafanya na yale yako mbele yake yanayohusu Taifa; mengine anaweza kuyamundu yeye kama yeye (Kama Kiongozi na Serikali yake) lakini mengine yako juu ya uweza wa kwake, juu ya uweza wa kibinadamu na hivyo yanahitaji maombi toka Mungu.

 1. KUOMBEA MAAFISA WOTE WANAOCHAGULIWA KWA KURA:
 2. KUOMBEA HAKI YA MAHAKAMA KUU NA MAJAJI:
 3. KUOMBEA JESHI:
 4. KUOMBEA MAISHA YA KIROHO YA TAIFA:
 5. KUOMBEA UCHUMI UWE IMARA
 6. KUOMBEA WAKUFUNZI, WAALIMU NA WANAFUNZI
 1. KUOMBEA JANGA LA UGONJWA WA KORONA (COVID-19)

Janga hili linawaangamiza zaidi wale watu ambao wamemuacha Mungu, waliomsahau Mungu kuliko wale waliomkimbilia Mungu. Taifa ambalo limemuweka Mungu mbele wanalindwa na Tanzania ni mmoja wapo (Tunalindwa) Tunajisifia Raisi wetu na najiskia fahari kumuunga Mkono. Taifa lile ambalo linafanya Mapenzi ya Mungu litaponyeka na ugonjwa huu. Kama anavyosema :-

ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao

2Nyakati 7:14

Uponyaji wa Nchi na majanga haya ambayo nimesema la ugonjwa huu pamoja na Uchumi, kama Mungu hajaridhia kuiponya Nchi hakuna awezae kuponya. Ugonjwa huu ni sehemu ya Hasira ya Mungu, hasira ya Mungu huwezi kuikimbia. Ugonjwa huu hauna cheo, Ukimuasi Mungu hasira yake inakuja juu yako. Nchi ya Tanzania Raisi amemtanguliza Mungu kwa maneno ya Kinywa chake na Matendo yake.

Tusikubali mtu yeyote, wa cheo chochote asiharibu msimamo huu ambao Raisi wetu amesema watu waombe! Tanzania tuko hapa, ni kwa sababu tuko Watakatifu tunafunga na tunaomba usiku na mchana. Ifuatayo ni nukuu ya Mtumishi wa Mungu ambayo nilimsikia akisema;

Mwaka jana Mungu alinionyesha jambo hili na nikasema ibadani kwamba kuna majanga yanakuja mbele yetu. Napenda kuwatangazia kwamba, hii ni dogo yake janga kubwa liko mbele yetu; linakuja lini sijui. Tutasimama kuomba Ulinzi na ulinzi wa Kwanza ni damu ya Yesu. Sisi tuna Mungu na tutangaza Mungu wetu.

Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira

Ukiendekeza uovo, uovu hautatoka nyumbani kwako, wapendwa tuombe, tusisubiri hali ibadilike tuombe sasa! Nasema tunaomba na tutaomba. Raisi tuko pamoja nawe songa mbele jina la Bwana libarikiwe.

 1. KUOMBEA ULINZI WA KIUNGU KWENYE ARDHI YETU
 2. KUOMBEA UMOJA NA MSHIKAMANO WA TAIFA
 3. KUOMBEA VYOMBO VYA HABARI
 4. KUOMBEA RAIA WA DUNIA

maombi

 1. Baba, kwa jina la Yesu ninaomba kwa niaba ya nchi yangu Tanzania, ninatubu dhidi ya ngono, uzinzi, umalaya, utoaji mimba, ubakaji, ujambazi, uuaji, dhambi za zinaa, tamaa, kukosa imani, husuda, wivu, uvivu, (taja kila uovu unaoujua). Tuponye dhidi ya madhara yatokanayo na mambo hayo.
 2. BWANA, taifa hili ni lako, kwa Jina la Yesu ninaomba umimine Roho yako juu ya taifa letu. Lete uamsho kwenye kila mji na kila kona ya nchi yetu na kwenye kila kanisa. Ninaomba katika taifa hili lisiwepo kanisa lisilo na uhai, bali yawepo tu makanisa yaliyojazwa na Roho wako.
 3. BABA, kwa jina la Yesu Kristo, naomba mkono wako wa ulinzi uwe juu ya rais wetu wa Tanzania (John). Naomba umlinde asidhurike ili afya yake na usalama wake daima uhakikishwe. Isiwepo silaha iliyo tengenezwa kwa ajili yake ikafanikiwa, naomba ulinzi kwa mke wake (Janeth) na familia yake dhidi ya kila magonjwa, ajali na kila maadui walinde kwa mbawa zako.
 4. Baba ulisema “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa” (Yakobo 1:5) kwa niaba ya Rais wa Tanzania, naomba umpe hekima, kupambanua na maarifa kwa maamuzi anayofanya. Mpe uvumilivu ili asije akajivuna, muongoze ili asije akakosea njia, mpe kibali kwa watu na viongozi wengine ili aleje umoja na sio utengano.
 5. BWANA, Umesema “Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana; Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo (Mithali 21:1)”. Ninaomba uugeuzie kwako moyo wa rais wa Tanzania wakati wote, katikati ya kelele nyingi anazozisikia kila siku, ili aweze kuisikia sauti Yako badala ya sauti za watu. Muongoze katika kila hatua.
 6. Baba, katika Neno lako umesema “Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele (Mithali 29:14)”. Kwa Jina la Yesu naomba kwamba rais wetu daima afanye lililo jema kwa watu wake. Msaidie awe rais asiyeshindwa kutembea katika kweli. Mfunulie daima inapotokea uongo unataka kumpotosha. Mfanye kila wakati atoe maamuzi kulingana na msingi imara wa Neno Lako ili daima awe kiongozi anayesimama kwenye msingi wa Neno lako.
 7. Baba kwa Jina la Yesu naomba kila mshauri wake wawe na hekima ya Mungu ili daima aweze kumpa mashauri mema. Waoneshe washauri wake unachotaka wafanye, waongoze kwenye maamuzi yote na wape majibu na ufumbuzi wa kila tatizo. Ninaomba kama kuna mshauri anampa ushauri mbaya rais wetu, umuondoe kwenye hiyo nafasi. Zaidi sana naomba waweze kuyatafuta mashauri yako na wasifanye lolote kinyume na mapenzi yako.

NYIMBO

 1. Ee Baba, Ee Baba Ee baba
 2. Nisememe nini Bwana
 3. Tenzi namba 15
 4. Wewe ni Bwana
 5. Jina lako linaweza Yesu
 6. Mwacheni Mungu

Sikikiza somo na Maombi haya kwa sauti live hapa

MFUNGO NA MAOMBI KUOMBEA TAIFA AUDIO / SAUTI

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s