Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
Mhubiri 3:1

Kama watoto wa Mungu, sio kazi yetu kujitimizia mahitaji yetu bali ni kazi ya Baba yetu aliye mbinguni ambaye anamiliki vyote na anajua majira na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu. Mungu hakutuumba tuhangaike bali aliumba kila tunachohitaji na kuweka duniani.
Ukimlingana Mungu sawasawa macho yako yataona, fahamu kuwa, kuna mahali ambapo Mungu amekuandalia wewe uliye wake. Je umepaona? Unahitaji Neno la Mungu ili macho yako yafunuliwe kwani mtu anayempenda Mungu, Mungu anasema naye kwa ndoto lakini manabii zake anasema nao waziwazi; kwa hiyo nenda ukaandamane na manabii zake kwa kuwa Mungu anawapa siri zake.
Amosi 3: 7 ” Hakika Bwana Mungu hatafanya Neno lolote, bila kuwafunulia, watumishi wake manabii siri yake”. Mungu amekuandalia watu wa kukusaidia kufungua macho kupitia mahubiri, mafundisho wanayotoa na vitabu walivyoandika, hivyo uwe mtu unayependa kusoma Biblia na vitabu vya watu wa Mungu waliofanikiwa.
Maombi
Mungu naomba unipe kujua kusudi la kuumbwa kwangu kwa kuwa mimi nimeokoka.