Ninamshukuru Mungu ambaye ametupa neema ya kuendelea kuliombea taifa letu la Tanzania na watu wa Tanzania. Mungu wetu anajibu maombi ya watu wampendao, ndiyo maana kasema:

“ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”

2 Mambo ya Nyakati 7:14

Danieli aliendelea kuomba kwa Mungu, ili Mungu asamehe na kuiponya Israeli na watu wake. Aliomba sana msamaha na kuomba Mungu awageukie tena watu wake kwa ajili ya uponyaji. Aliomba sana msahama na marejesho lakini alikuwa muwazi mno kwenye mambo ambayo alitamani Mungu awasamehe na kuweza kuingilia kati kuleta uponyaji wa taifa lake: Alisisitiza mambo haya:

 1. Kusikilizwa maombi yake: Jambo zuri sana ambalo lilimfurahisha Mungu katika ombi hili ni pale alipojitambulisha kuwa yeye ni mtumishi wake na akasema iponye Yerusalemu kwa ajili yako Bwana. Na hili ndilo ombi ambalo pia Bwana Yesu aliwafundisha wanafunzi wake aliposema salini hivi “… Mapenzi yako yatimizwe ..”. Ninajifunza kwamba kila tunapomwendea Mungu kwenye maombi tuhakikishe tunaomba jambo ambalo lina manufaa kwake, maana sisi tu watumishi wake tu hatuna vya kwetu, vyote ni vyake.
 2. Kutaka Mungu afungue macho aone ukiwa: Danieli alipoona mateso ya watu yanazidi, akasema Mungu Baba fungua macho yako tuone ambavyo tumefanya uovu lakini tulipoishia ni maumivu mengi, tumekwa na tunajisalimisha kwako. Na ikumbukwe yeye kama kiongozi wa serikali akasema Bwana hata tunaomba utusaidie dhidi ya watu wako maana ukitazama kwa akili zetu tumeshindwa.
 3. Kumtaka Mungu atumie huruma / rehema na siyo haki: Utabaini kuwa Danieli alishajua kwa kuwa Mungu ni mwenye haki, tayari yanayoendelea katika nchi ni sahihi kabisa, akaona ni vema kukata rufaa kwenye mahakama ya rehema. Maana rehema inakupa kitu ambacho kwa hali ya kawaida hukustahili bali kwa mapenzi ya atoaye – rehema ni pendo la Mungu kwa wenye dhambi, linalotangaza msamaha na kuhesabiwa haki. Na hata sisi tunahitaji sana rehema za Bwana kwa ajili ya Mungu kuwaponya Watanzania na nchi kwa ujumla. Kwa vyovyote iwavyo, Mungu ni Baba yetu tuwe tumemkosea au la, tunahitaji msaada wake.
 4. Asikie maombi na kusamehe bila kukawia: tunajifunza jambo la ajabu sana hapa Danieli ana ujasiri sana anamlilia Mungu akisema sikia, samehe na utende kwa ajili yako mwenyewe Mungu. Ni kweli kwamba Mungu bado anatupenda sana licha ya kuishi maisha ya dhambi, uasi na uovu – kwa kujua hili ndiyo maana tunahitaji kumuomba Mungu atusamehe haraka ili lile pendo lake kwa watu wake na taifa alione likichanua kwa upya.

maombi

 1. Ee Baba, kwa jina la Yesu Kristo tunashukuru kwa maana tumejua kuwa wewe ni mwenye haki na una hukumu kwa haki daima. (Zaburi 119:7)
 2. Baba tunaomba kusikilizwa kwa maombi haya, watumishi wako tumefunga na kujinyenyekesha kwako, turidhie Baba usiharibu watu wote na nchi yetu Tanzania (Mwanzo 18:26-32)
 3. Baba, kwa Jina la mwanao mpendwa Yesu Kristo, tunasihi huruma zako Bwana na rehema kwa ajili ya taifa letu la Tanzania na watu wake wote, maana kwa haki tunastahili kuangamia. (Zaburi 145:8)
 4. Ee Baba tunaomba kwa jina la Yesu Kristo, utujibu bila kukawia, tunakusihi sana hasa wakati huu ambao taifa zima linangojea msaada wako (Danieli 9:19).

Sikiliziza somo hili kwa SAUTI MAOMBI YA KUJIPATANISHA NA MUNGU IV

NYIMBO

 1. TENZI NAMBA 24
 2. NI WEWE MWENYE UWEZA, TWAKUKIMBILIA WEWE,
 3. NINAMJUA YEYE ALIYENIUMBA.
 4. WATUJUA VEMA BWANA
 5. MWAMBA NI YESU

2 thoughts on “KUJIPATANISHA NA MUNGU IV

 1. Amina baba Mungu akubariki kwa masomo mazuri,akupe nguvu na uwezo ktk kutufundisha wanao maana tunahitaji kujifunza na kujipatanisha Mungu.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s