Haleluya! Leo ni siku ya tatu ya mfululizo wa maombi ya siku saba kwa ajili ya upatanisho wa Tanzania na Mungu aliyeiumba Tanzania na watu wake – aitwaye NIKO AMBAYE NIKO.

“Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; 5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; 6 wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi. 7 Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa. 8 Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi. 9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; 10 wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii. 11 Naam, Israeli wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako; basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na uapo ule ulioandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi.”

Danieli 9:4-11

mAMBO AMBAYO HATUNA BUDI KUYAZINGATIA

  1. Alianza maombi kwa kutambua ukuu wa Mungu: Uombaji wa Danieli ulizingatia itifaki ya Mungu, unakumbuka hata Yesu alipokuwa anawafundisha wanafunzi wake aliwaambia salini hivi “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe”. Na akasema tunatambua Mungu huvunji maagano ila sisi wanadamu ndiyo wenye matataizo maana tunavunja maagano.
  2. Kukubali kosa kuwa sote tumetenda dhambi: ukisoma (Danieli 9:5,8,11 na 15) utabaini kuwa anaomba msamaha kwa ujumla wake, haombi kwa ajili ya wenye dhambi pekee. Amejijumlisha kwenye kundi la watu wote bila kujali ni Rais, viongozi wakubwa au viongozi wa kiroho ama watu wengine. Na sisi lazima tuwe hivyo, tuliombeee taifa letu la Tanzania bila kunyosha vidole kwa wengine. Jambo la namna hii linaufurahisha moyo wa Mungu.
  3. Kutoamini watumishi wa Mungu: Unajua mabaya ambayo yaliwapata wana Isreali Nabii Isaya na Yeremia walishatoa maonyo mapema siku za Mwanzo. Kama wazee wangekubaliana na mashauri ya manabii nchi isingefika hapo ilipofikia. Na hata sisi pia lazima tukubali kuwa Mungu anaogea na watumishi wake katika taifa letu inawezekana mpaka leo tunafika hapa kuna hali ya kupuuzia mausia ya watumishi wa Mungu.
  4. Mungu ni mwenye haki: Hawezi kupiga taifa kama hapana ouvu unaondelea kwenye hilo taifa. Ni wachache sana wenye uwezo wa kujua sasa tunafanya uovu. Na hakuna uovu mkubwa kama kuabudu miungu mingine. Katika nchi yetu wapo watu wengi bado wanaamini hawawezi kusoma, kufanya biashara, kupata vyeo bila kwenda kwa waganga wa kienyeji – na huku ndo kuabudu miungu mingine.
  5. Haya au aibu: Hii iliwakuta kwa sababu wanajua Mungu anataka nini na wao wanafanya nini, uzuri ni kwamba tunapokuwa na tabia mbaya za uovu ujasiri wa kuongea na Mungu unaondoka kabisa. Tukifikia hatua ya kuona haya kuja mbele za Mungu tambua kuwa sasa mabaya yameruhusiwa kwetu.

MAOMbi

  1. Baba wa Mbinguni, uinuliwe na kutukuzwa mno kwa kuwa unauwazia mema tu sisi Watanzania. tunashukuru maana tunajua kuwa una mpango mwema na nchi yetu na kila Mtanzania.
  2. Baba, kwa Jina la Yesu Kristo tunaomba uturehemu sisi Watanzania maana tumefanya dhambi, ukaidi na tumetenda maovu mbele zako na tumeasi na kuacha njia yako. Samehe Baba!
  3. Baba, kwa Jina la Yesu tunaomba utusamehe maana hatuwasikilizi watumishi wako manabii, kwa sababu hiyo tunajikuta katika hali ya kuangamia. Tunaomba rehema zako na neema ya kusonga mbele kwa kukupendeza Wewe.
  4. Eeh Mungu Baba, uliye mwenye haki, tunaomba utuhurumie maana tumejaa haya kusongea mbele zako kwa sababu makosa yetu yanatufukuzia mbali nawe.
  5. Baba tunaomba Tanzania ipate rehema zako, viongozi wetu wapate rehema zako, na Watanzania wapewe kibali mbele zako ili tuwe furaha yako.

Unaweza kusikiliza somo hili hapa:

https://web.facebook.com/boniemwa/videos/2357070871259299/

Karibu kwa maombi.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s