Kwa ujumla ni kama nilivyoeleza jana kuwa Mungu anatupenda sana na ahataki kuona tunapotea hata kidogo, ila ameruhusu maamuzi yawe ndani yetu sisi wenyewe kuamua kupotea au kusalimika mikononi mwa Mungu. Tunasoma Yohana 3:16-19

16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. 18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.

Mpango wa Mungu tangu mwanzo ni mtu yeyote asipotee kwa majanga, magonjwa au njaa ndiyo maana ameweka njia ya kututoa katika maangamizi ambayo ni Yesu. KUmbuka Yesu mwenyewe anasema ndiye njia, kweli na uzima (Yohana 14:6). Ni vema tukatambua kuwa hatuna mpatanishi mwingine awezaye kutupatanisha na Mungu Baba isipokuwa Yesu.

yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.

2 Wakorintho 5:19

Daniel ni mmoja kati ya watumishi wa Mungu ambao hata hawakuwa manabii, lakini alichoamua kufanya baada ya kuona taifa lake la Isareli linazidi kupitia magumu akarudi kusoma vitabu ili ajue Mungu aliahidi nini na kwa wakatai gani.

katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini

Danieli 9:2

Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.

Danieli 9:24

Jambo la msingi sana kuliangalia hapa siku ya leo ni hatua ambayo Danieli aliichukua baada ya kuona taifa linapitia ukiwa na hali ya kutojua nini cha kufanya: Tunaona hatua kadhaa kama tunavyosoma: –

Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.

Danieli 9:3
  1. Alibaini kuwa tatizo ni makosa ya watu kwa Mungu
  2. Akautafuta uso wa Bwana ili kusababisha upatanisho
  3. Alifunga na kuomba kwa unyenyekevu mno.

MAOMBI

  1. Baba tunashukuru kwa kuwa unajibu maombi yetu kila tunapo-omba kwa ajili ya taifa letu la Tanzania (Wafilipi 4:6).
  2. Baba, kwa jina la Yesu tunashukuru umelitunza taifa letu tangu kipindi cha uhuru mpaka leo (Maombolezo 3:22)
  3. Baba, kwa jina la Yesu, tunashukuru kwa kila uhuru na raha ambao kanisa lako la Tanzania limekuwa likipata tangu ulipolianzisha hadi sasa kwa maana unalilinda kwa malaika wako daima. Zaburi 34:7
  4. Baba, kwa jina la Yesu, ruhusu msamaha wako kwa kila makosa na uovu wetu Watanzania mbele zako. 2 Nyakati 7:14
  5. Ee Baba, kwa jina la Yesu, tunaomba mabaya yasipate nafasi ya kuiangamiza nchi yetu Tanzania, tunajiitisha kwako kwa kukuambia hatuna Mungu mwingine ila Wewe pekee. 2 Nyakati 7:22

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s