Pastor Boniface
Maombi yanatupatanisha na Mungu

Katika maisha tunayoishi tunahitaji sana kujikagua kama tunatenda sawa na mpango wa Mungu au tumetoka kwenye reli. Kila wakati tutambue kuwa tunahitaji kuomba mapenzi ya Mungu yatimie kwenye maisha yetu iwe ni binafsi, kifamilia, kiukoo au kitaifa.

MAMBO YA NYAKATI 7:12-15 "Bwana akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. 13 Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; 14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa."

Utajuaje kuwa Mungu amekukasirikia au ameikasirikia nchi yako?

  1. Ukame: maana amesema atazifunga mbingu zisiweze kunyesha mvua, pasipo mvua hakuna ubichi au maji hiyo kupelekea ardhi kutolimika na kutoweza kupanda chochote. Kumbuka kuwa Mungu alipoumba mwanadamu alimuweka katika bustani yaani katika nchi na akampa agizo la kuilima na kuitunza.
  2. Njaa: amesema ataamulu nzige kula nchi, hii ina maana kuwa tukikosa adabu mbele zake Mungu anaamuru wadudu wabaya ambao waweza kuwa nzige au ndege wa aina yoyote kuvamia kila aina ya mazao amabayo mwanadamu anayategemea, ili tu aishi kwa njaa maana ameacha njia za Mungu.
  3. Magonjwa ya Mlipuko: Ukiona magonjwa mabaya huku duniani yanijitokeza tambua kuwa Mungu amekasirika kutokana na watu wake kutenda mabaya mengi, mfano: kuoana kwa jinsia moja, kutoa mimba na mauaji yasiyo na tija. Mungu akiona watu wake wanazidi kutenda mambo ya kishenzi kama hayo na yafananayo anatuma magonjwa yanayooangamiza jamii hiyo (anatuma tauni).

Utaona moja kati ya haya au yote kwa pamoja:

Tunawezaje kujiponya au kuiponya nchi yetu?

Mungu ni mzuri sana na ameweka wazi kila kitu ambacho kitatusadia kuweza kufanikiwa kutimiza mapenzi yake. Yafuatayo lazima tuyafanye ili tuweze kujipatanisha naye na kusababisha uponyaji wetu na familia zetu na nchi kwa ujumla:

  1. Kukubali wito wake: Kumbuka kuwa Mungu anatuita ili tuweze kuwa watumishi wake huku duniani, tuweze kuwa mabalozi wake na wawakilishi wa ufalme wake. Tunatakiwa kujitambua kuwa sisi ni wana wa Mungu, tumekusudiwa kuyatenda mapenzi yake na sio tunayotaka sisi, lazima tuwe na kiasi katika utendaji wetu huku tukijiuliza je kwa hili Mungu atanifurahia au atanikasirikia. Kwa nafasi yoyote uliyonayo uwe Rais au waziri, uwe mbunge au mkuu wa idara, uwe mwalimu au polisi uwe mfanyabiashra au mchungaji lazima utambue hiyo kazi Mungu amekuita uifanye kwa niaba yake – tekeleza kwa hofu ya Mungu.
  2. Kuamua kunyenyekea: yaani kuishi kwa kujishusha kwa aliye juu yako. Na kila mwanadamu lazima ajishushe kwa Mungu kwa sababu haijalishi una utajiri kiasi gani au cheo kikubwa namna gani tambua kuwa wewe ni mdogo kuliko Mungu. Mungu akiona unajua kunyenyea kila mamlaka iliyowekwa basi anajua sasa amepata mtumishi anayestahili kuaminiwa. Kila kiburi, majivuno, kujisifu kwingi kunapelekea kuwasha hasira ya Mungu. Kufunga ni sehemu ya unyenyevu kwa Mungu wetu – yaani unashinda na njaa kwa masaa kadhaa au siku kadhaa ili mwili wako ukose nguvu na roho yako iweze kupata nguvu ya kuutawala mwili kwa manufaa ya kutumiwa na Mungu.
  3. Kuomba: Maisha ya maombi yanampendeza sana Mungu kwa sababu unaonesha kuwa unatambua ubaba wake, uatambua uwezo wake, unatambua kuwa yeye anaweza yote. Mungu anatamani kwa kila jambo tuombe kwake ili atupe usaidizi. Unaweza kuomba kama unaona tabia yako inakuwa mbaya ili akupe neema ya kubadilika, unaweza kuomba kwa ajili ya maisha yako, kuomba msamaha, kuomba akupe kazi na mengineyo.
  4. Kuutafuta uso wa Mungu: Hii ni hatua ya maamuzi ya kuamua kuijua sheria yake, kuzijua kanuni zake na amri zake. Unapoamua kusoma au kusikiliza Neno la Kristo kwa bidii na kuzingatia kutenda sawasawa na sheria zake, huko ndiko kuutafuta uso wa Mungu. Kwa lugha nyepesi nikwamba, Mungu anaficha uso wake kwa watenda dhambi na anajifunua kwa wale ambao wameamua kuishika sheria yake na kuitafakari mchana na usiku maisha yao yote. Ukiona mambo mabaya yanakukablili au kuikabili jamii yenu au nchi yenu chukua hatua ya kurudi kwenye sheria zake na ukigundua uko nje ya utaratibu omba Mungu akusamehe na kuanza upya na wewe maana anapenda mapatano na watu wake.
  5. Kuacha njia mbaya: ni hatua ya muhimu sana kama unataka Mungu afanye mambo mapya, aondoe hasira na ghadhabu yake juu ya nchi au familia au kwako. Njia mbaya ni kama usingiziaji, wizi, ufilaji, matusi, ulevi, uchoyo, uuaji, fitina, nia mbaya, ubinafsi, ufisadi, ujeuri, kutunga mabaya, kutoheshimu wazazi au wakubwa na mengineyo mengi. Ndiyo maana akesema

Warumi 1:28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.

Kukubali kuacha njia mbaya ni kukubali kuwa na Mungu katika fahamu zetu. Na hili linawezekana tu kwa kusikia Neno la Mungu (Warumi 10:17) na kufanywa watu wa imani kama alivyosema haiwezekani kumpendeza Mungu pasipo imani (Waebrania 11:6).

MAOMBI

  1. Baba Mungu, kwa jina la mwanao Yesu Kristo na Kwa Damu yake Yesu naomba unisaheme makosa yako yote, naomba unioshe kwa damu Yesu ili nianze kwa upya na Wewe.
  2. Eeeh Baba yangu uliye Baba wa mababa wote naomba unifanye kuwa rafiki yako. Naomba uniridhie tuwe marafiki, nimechoka kuwa peke yangu nimegundua wewe ni rafiki wa kweli. Henoko alikuwa rafiki yako, Musa alikuwa rafiki yako na mimi natamani niwe rafiki yako.

2 thoughts on “KUJIPATANISHA NA MUNGU

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s