Matendo ya Mitume 24:16 “Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote.”

Kanisa la Kristo duniani litakuwa na afya sana endapo wakristo wote watakuwa na dhamiri ya wazi ya kuogopa kufanya makosa. Cha ajabu ni kwamba mara kwa mara makosa mengi sana yanajitokeza katika mwili wa Kristo. Hii inatokana na kutumia vibaya fursa tupatazo, utajiri na vitu tunavyo miliki.

Ili kupanda mema kanisani ni lazima tufuate kanuni za kiroho ambazo Mtume Paulo alituwekea katika 1 Timotheo 6:17-18:

Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. 18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;”

Namba kubwa ya Wakristo bado wanaishi chini ya kifungo cha dhamiri iliyo jaa hatia. Kwa nini? Ni kwa sababu hawajaamua kuachana na ukale wao kabla wa wokovu. Mfano, utakuta mtu kaokoka lakini bado anaishi na mwanamke ambaye si mke wake wa kwanza. Wengine bado wanaishi kwenye nyumba ambazo walijenga kwa fedha za uizi au dhuruma. Wengine wanaona ni kazi kuzuia mahusiano yao na makundi au marafiki wenye vikao vya kishetani.

Hayo na matatizo mengine mengi ni vikwazo vinavyosababisha watu kupata uhuru kamili. Baadhi ya watu wa namna hii huwaweka wachungaji wao kwenye kibano, kwa sababu matatizo yao yanagoma kuondoka. Hivyo huonesha kuwa pengine Mchungaji hana upako wa kutosha kukabiliana na matatizo yao. Hivyo utakuta wana hama kanisa mara kwa mara ili kupata kanisa ambalo atapata raha dhidi ya matatizo yake, lakini bado hawapati raha ya roho zao.

Matumizi mabaya ya mali na nafasi, hasahasa yale yaliyo mali au nafasi vilivyopatikana kinyume cha sheria, hukwamisha sana uhuru wa dhamiri. Ndiyo maana maisha ya amani, furaha na ridhaa yaliyotegemewa, ambayo ndiyo tegemeo letu kubwa tunapo okoka na yanayotufanya kuwa wa kipekee kama wana wa Mungu, yametuepuka kwa hila.

Kuna msemo usemwao sana na Wakristo wanaoshutumiwa kwa matumizi mabaya ya mali na nafasi zao usemao “Dhamiri yangu hainihukumu mimi.” Swali ni: dhamiri ipi hiyo unayoiongelea? Ni ile ya wafu waliokataliwa? Baadhi yao hudiriki hata kusema “Wale wote waongozwao na Roho, hao ndiyo wana wa Mungu.” Roho gani unayoingelea? Inaweza kuwa roho ya Mungu, ambayo iliyovuvua uandishi wa Neno la Mungu na ikageuka leo kuwa kile roho wa Mungu aliwaoongoza watu kuandika ilikuwa ni makosa?

Mpendwa tusijidanganye wenyewe zaidi ya hapo. Tuamue kuishi maisha ya Kikristo, maisha yanayo tutoa kunako hatia dhidi ya Mungu na watu, na hasahasa wale watu wa nyumbani katika imani.

Warumi 14:16-21 “Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya. 17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18 Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu. 19 Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. 20 Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza. 21 Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.”

Omba: Baba kwa Damu ya Yesu, niondolee makosa na dhamiri mbaya ya kazi zangu zote zilizokufa ambazo huniletea hatia, katika Jina la Yesu.

One thought on “Dhamiri Ya Wazi Isiyo na Hatia

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s