Wakolosai 3:2 “Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.”

Nimebaini kuwa wakiristo wengi wanashindwa kuishi maisha ya viwango vya maagizo ya Biblia kwa sababu wanapenda sana vitu vya duniani kuliko vya mbinguni, na sababu ya hili ni kutokana na kuja kwa kupenda utajiri wa mali kama kanisa. Naweza kuwa je ni makosa kuwa tajiri? Hapana! Ibrahim alibarikiwa sana, Isaka alibalikiwa sana na Yakobo pia alibarikiwa sana. Na bado hawa wote walimtumikia Bwana. Mfalme Daudi alimbariki BWANA kwa ustawi wa vitu pamoja na vingine vingine.

Zaburi 103:1&5 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;”

Hivyo napenda kusema neema unayohitaji ili kutawala utajiri wa vitu ni kubwa kuliko ile ya kutawala umaskini. Mungu anapoanza kukubariki lazima uzidi kuomba kwa bidii sana ili kutawala ustawi wako kinyume na hapo mapenzi au upendo wako utahama toka vitu vya mbinguni na utapenda vya dunianiani sana.

Ni upumbavu wa hali ya juu sana kumpenda na kumtumikia Mungu wakati u maskini wa vitu vya duniani, unakuta mtu anamsahau Mungu akipata mali aliye mpa nguvu za kupata utajiri. Ndiyo maana Biblia inasema;

MITHALI 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.”

Wana wa Mungu wengi sana wakati wana hangaika kupata kipato walisema “Baba ufalme wako uje” lakini baada ya kufanikiwa wanaishi maisha kama vile hawatakufa kamwe, na kama vile Yesu hata kuja wakati wowote. Si kazi ngumu kabisa kuwabaini watu ambao upendo wao uko kwa vitu vya mbinguni, kwa sababu saa zote utawaona wako na kazi ya kujenga na kuupanua ufalme wa Mungu. Kwa sababu uwekezaji wao ni wa Mbinguni, na mioyo yao muda wote inawaza juu wa mbinguni.

MATHAYO 6:20-21 “bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; 21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”

Hakuna uhakika wa hazina unayoitunza na kuweka duniani. Uwekezaji wako katika vitu vya mbinguni ndicho utakachobaki nacho baada ya kuingia mbinguni. Hivyo basi, anza kuweka matamanio juu ya vitu vya mbinguni tangu sasa.

Soma: Wakolosai 3:1-6 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. 5 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; 6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.”

Omba: Mpenzi Roho Mtakatifu, jaza moyo wangu na upendo kwa ajili ya vitu vya mbinguni katika Jina la Yesu.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s