MHUBIRI 5:10 “Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba maongeo. Hayo pia ni ubatili.”

Gehazi alikuwa ni mtumwa wa nabii Elisha. Alipewa nafasi ya kuwa mwanafunzi wa nabii mkubwa na alikuwa na nafasi ya kurithi ule upako wa mara mbili wa nabii Elia uliokuwa juu ya Elisha. Ingawa tamaa zake ziliikimbiza hatma yake ya kuwa nabii mkubwa sana hapo badaye. Aliamua kumtafuta vitu vya kila siku vya dunia hii kwa gharama ya wito wa kinabii alioupata. Alikuwa na mtazamo wa vitu vya kidunia sana na hata akaapa mbele za Mungu kuwa lazima “amiliki vitu / mali”. Kama wahubiri wa siku hizi, ni kama alisema “… anayefanya kazi madhabahuni lazima ale vya madhabahuni” zingatia maneno yake 2 Wafalme 2:20

“Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake.”

Baada ya dhambi yake ya tamaa kujulikana na bwana wake, ukoma wa Naamani ukahamia kwake na vizazi vyote baada ya yeye (2 Wafalme 5:27)

Yuda Iskarioti ni mfano wa mtu mwingine ambaye tunapaswa kujifunza kwake. Alikuwa na maadili na matatizo ya kiroho kama vile Gehazi; tamaa na mlafi. Biblia inasema kwamba alikuwa mwizi, na licha ya kuwa Mhasibu wa Huduma ya Yesu mara nyingi aliiba katika mfuko wa fedha (Yohana 12:4-6). Ulafi wake ulimfikisha hatua ya maamuzi yaliyo mpelekea hatia ya Kukosa uzima wa milele; aliamua kumuuza Bwana wake, mfalme wa Utukufu (Mathayo 26:14-16). Kabla Yuda Iskariote hajatambua ujinga wake, alijipotezea nafasi ya kuhesabika miongoni mwa Mitume kumi na mbili. Aliishia kujinyonga.

Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. 5 Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.” Mathayo 27:3&5.

Wana wa Mungu katika nyakati hizi lazima wawe na hofu na vitu vya kidunia. Vinaua, Ingawa huwezi kugundua haraka. Ndiyo maana Yohana mpenzi wa Yesu alituonya walimwengu kama vile alijua kanisa litakavyokuwa siku za mwisho (1 Johana 2:15-17.

Omba: Baba, niongoze kamwe nisije nikafanya maamuzi ambayo yataweka giza katika ubadaye wangu katika Jina la Yesu. Amen.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s