MWANZO 25:32 “Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi?

Wakati maamuzi yaliyofanywa njiapanda yalipelekea ubadaye mzuri kwa Musa, Elisha, Danieli, Petro, Paulo na Ruthu maamuzi ya Esau akiwa njiapanda yakampelekea kuharibu ubadaye wake kisa chakula (mahitaji ya sasa) akabadirishana na haki ya mzaliwa wa kwanza (mali ya badaye). Esau alikutana na hatua mbaya sana ya kugeuka kwa kuuza haki yake. Alishibisha tumbo lake, akanywa na kusaza, akaamka na kwenda mbali, lakini alibaki na majuto ya milele. Biblia katika Waebrania 12:16-17 inasema

Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja. 17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.”

Mtu mwingine aliyechukua maamuzi mabaya katika hatua ya kugeuka ni Reubeni, mtoto wa kwanza wa Yakobo. Alikinajisi kitanda cha baba yake kwa kulala na suria wa baba yake aliyeitwa Bilha. Reubeni alipofanya maamuzi haya alidhani anamkomoa baba yake pasipo kujua kuwa alikuwa anaharibu maisha ya ubadaye wake.

Baba yetu wa mbinguni anastahili heshima yetu na si kumuumiza. Tuna muumiza sana Mungu tunapomfanyia ibada ambazo zimechanganyikana na tabia za kidhambi (Malaki 1:6-7). Kama makuhani wa Mungu (Ufunuo 1:6), tunaponyoosha mikono isiyo na utakatifu kumwabudu Mungu, tunatoa ibada chafu katika madhabahu yake. Ndiyo maana katika Biblia kitabu cha Warumi 12:1 amesema

“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”

Kitu cha kuogopesha sana katika stori ya Reubeni ni kwamba alipofanya hili tendo haramu, hukufahamu kama baba yake amejua. Kwa sababu baba yake hakuwahi kulizungumzia hata siku moja (Mwanzo 35:22) ingawaje siku ya hesabu baba yake alimlaani Reubeni kwa kosa la kunajisi kitanda.

Hivyo ninakushauri uombe juu ya mapenzi ya Mungu kwako, kupitia damu ya Yesu Kristo, ili baba wa Mbinguni akuondolee kila tendo ulilolifanya hapo nyuma ambalo mpaka sasa linaleta mashaka juu ya Ukristo wako.

Omba: Baba, tafathari niondolee kila uovu niliofanya wakati wa ujinga ambao umeweka laana juu yangu.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s