RUTHU 1:16 “Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;”

Baada ya Ruthu kupoteza mme wake mapema sana katika maisha yake na hakuwa na mtoto wa kumfariji, hakuweza hata kuota kama atakuwa mama wa mataifa kupitia Yesu Kristo, Bwana wetu (Mathayo 1:5). Ruthu huyu alifanya maamuzi mazito sana ya Kufuatana na mama mkwe wake Naomi licha ya kifo cha watoto wa kiume wa Naomi, lakini Orpa yeye aliamua kuaondoka.

Ruthu alisema maneno mazito kama ulivyosoma hapo juu. Lakini baada ya kuhamia nchi ya Israeli Ruthu akaolewa na Boazi ambaye alikuwa ndugu wa mbali wa marehemu mmewe. Huu uamuzi wa Ruthu ukapelekea kuzaliwa kwa Obedi ambaye ni shina la ukoo wa Bwana Yesu maana Obedi ndiye baba yake Yesse (Ruthu 4:13-17).

Kila wakati nakumbuka uamuzi niliochukua kumtumikia BWANA katika Huduma ya Efatha, ninampa sifa na utukufu Bwana wa mabwana. Pale nilipochukua hatua ya kuachana na kujihesabia haki na kujiona msomi, nilijua kuwa naingia kunako nafasi kubwa ya furaha ya Bwana maana nilijua hakuna ajira kubwa duniani kama kuajiriwa na Mungu. Nanamshukuru roho Mtakatifu aliyenisaidia kufanya maamuzi haya makubwa. Nakuombea kwa Bwana akujalie na wewe kufanya maamuzi yenye ubadaye mwema kwako, katika Jina la Yesu Kristo. Ili uamue kumtumikia BWANA katika roho na kweli tangu leo katika Jina la Yesu Kristo.

Mara ya mwisho Biblia kumtaja Orpa ni pale alipofanya maamuzi mabaya akiwa njiapanda, maana alifanya maamuzi ya kurudi kuabudu sanamu.

RUTHU 1:14-15 “Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthuu akaambatana naye. 15 Naye akasema, Tazama, shemeji yako amerejea kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urejee wewe umfuate shemeji yako.”

Mpendwa, ni hali gani ambayo unapitia sasa, ni magumu gani unayatengeneza. Umepima maamuzi unayoyachukua? Je, Mungu umempa nafasi yako katika taswira yako? Tafakari hili na nenda kumuomba Mungu akujalie.

Omba: Roho Mtakatifu, tafadhari niongoze kufanya maamuzi sahihi kila wakati niwapo njiapanda.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s