Hatua ya kugeuka ni hatua ya kujitambua, ni hatua ya maamuzi ambayo hutengeneza ama kuharibu maisha ya mtu. Katika safari ya maisha daima kuna njiapanda nyingi sana ambazo zinamsumbua mtu kuamua kwenda kulia au kushoto. Katika hatua hii ukifanya maamuzi sahihi utukufu kwa Mungu na ukifanya maamuzi mabaya, Mungu akurehemu.

Biblia inaonesha watu wengi waliofanya maamuzi sahihi na yale mabaya pale walipokuwa njiapanda. Musa ni mfano wa watu hao. Musa alifanya maamuzi ambayo si tu yaliokoa maisha yake bali pia ya Wayahudi wote. Nakuombea nawe leo fanya maamuzi sahihi ambayo yatakuokoa wewe, ndugu zako na jamii yako yote hapa duniani, katika Jina la Yesu Kristo nimeomba.

KUTOKA 3:3 “Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.”

Hapo juu tunasoma vile Musa alivyoamua kugeuka mara tu alipoona maono. Akageuza nia yake ya kawaida na kufuata aonacho. Ukiendelea kusoma utagundua kuwa Mungu alianza Kuongea na Musa mara tu alipoamua kugeuka na kisha Akampa jukumu la Ufalme wa Mungu (Kutoka 3:10).

Mtu mwingine ambaye alifanya maamuzi sahihi ya kugeuka ni Elisha. Uliamua kugeuka kuacha kuchunga na kumfuata Nabii Elia ili amhudumie (I Wafalme 19:19-21) na maamuzi yake hayo yalimpelekea kuitwa na wafalme “baba”.

Maamuzi mengine ni ya Danieli, alipoamua kuwa yeye na wenzako hata jinajisi kwa chakula cha mfalme “nyama” ilimpelekea kujulikana na wafalme wote na kuwa mtu wa mfano kwao wote. (Daniel 1:8, Danieli 1:21, Danieli 5:11-12). Siku Petro alipoona maajabu ya kuvua samaki wakati Bwana Yesu kamwagiza aliamua kutii agizo akageuka toka kuvua samaki sasa akaanza kuvua watu (Luka 5:10-11, Matendo 5:15).

Maamuzi ya kugeuka aliyoyafanya Paulo barabarani akielekea Dameski yalipelekea kuwa mtu mkuu sana ambaye mpaka akafikia kutandika zaidi ya robo tatu ya vitabu vya Agano Jipya, bila kusahau miujiza mingi sana ambayo Bwana Yesu alimtumia kuifanya (Matendo 9:3-8, Matendo 19:11-12).

Je wewe umeamua kumgeukia Yesu ambaye yeye ni njia kumfikia Mungu? Fanya maamuzi sahihi ili usicheleweshe muujiza wako na jamii inayokuzunguka. Maamuzi yako yamebeba kusudi la Mungu. Fanya maamuzi sahihi ya kuokoka na kama umeokoka acha maagizo basi fanya maamuzi ya kumaanisha wokovu wako. Mungu ataingilia kati maisha yako na kuitengeneza akili yako ili umtumikie katika roho na kweli.

Ombi: Mwambie Mungu, nafanya maamuzi sahihi kukutegemea kwa maisha yangu ya miaka yote iliyobaki hapa duniani. Na omba Mungu akupe kusimamia uamuzi wako huo katika Jina la Yesu Kristo Amen.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s