2 Wakorintho 14:27 “katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.”

Hii ina maanisha kuwa unapolipa gharama kwa maumivu makubwa katika Uhusiano wako na Mungu na katika huduma, utahamishiwa viwango vya juu vya upako. Gharama ikilipwa si tu kwamba utaona visivyo onekana bali pia utasikia visivyo sikika.

1 Wafalme 18:41 “Naye Eliya akamwambia Ahabu, Haya! Inuka, ule, unywe; kwani pana sauti ya mvua tele.”

Wakati wengine waliendelea kujadili juu ya moto ulioshuka toka mbinguni ghafla Elia akaamka na kuamuru sauti ya mvua. Elewa kuwa hapa hakuna mwingine alisikia wala kuona dalili ya mvua.

Kuanzia leo utasikia visivyosikia kuanzia leo katika jina la Yesu! Ingawaje kufikia kiwango hiki ni lazima uwe mtu wa kufunga na kuomba. Ndiyo maana Mtume Paulo anasema “katika kufunga mara nyingi”.

Tangu unapoamua kutumika kikamilifu mbele za Mungu vita ya mwili na roho inaanza kwa viwango vipya. Wakati mwili unakusukumia kushoto roho inakusukumia kulia. Unahitaji kufunga ili kudhoofisha mwili na kuipa nguvu roho yako.

Yohana 6:63 “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”

Kutumia mkono wa mwili wakati huu utaishia majuto bali tu ule mtembeo wa kiroho utakupelekea kuongozwa na Roho Mtakatifu; hii humpa nguvu mtu wa rohoni na huutiisha mwili. Kama huna nguvu ya kutawala hamu ya kula au tumbo lako sahau kukutana na miujiza ya Mungu au kutenda maajabu ya Mungu.

Mathayo 17:14-21 “Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, 15 Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. 16 Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. 17 Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. 18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. 19 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. 21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]”

Tunapata mwanga kuwa kwa kufunga na kuomba kila matatizo yanatoweka.

Pointi: kama unataka matokeo ya mbinguni, lisha roho yako. Kama unalisha mwili wako utazaa dhambi maishani mwako.

Kwa uelewa zaidi sikiliza audio hii hapa. Amen
KUFUNGA NA KUOMBA NI MUHIMU

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s