Marko 16:17 “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;”

Kutoka Marko 16:17, tunaelewa kuwa ishara na maajabu zinawafuata wale waliaminio Jina la Yesu Kristo. Nguvu itendayo maajabu katika jina la Yesu pia imezungumziwa katika Isaya 9:6

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.”

Ni kweli Jina la Yesu lina maajabu mengi na makubwa, Mtume Petro alisema katika Matendo ya Mitume 3:6;

“…Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.”

Ghafla Petro akalitaja Jina la Yesu, miguu na mifupa ya kilema aliyekuwa akiongea naye ikapokea nguvu na ikaanza kufanya kazi vizuri akaanza kutembea na badaye kurukaruka. Ukiwa na Jina la Yesu mdomoni mwako, hakuna kinachoweza kushindikana kwako. Wale wasio liamini Jina la Yesu kwa wokovu, labda kwa sababu ya dini zao au usomi wao, hajajua wamepungukiwa nini kwa kulikosa jina la Yesu. Biblia inasema:

Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.” –Mithali 18:10

Hilo andiko linafunua siri nyingine ambayo inalipelekea Jina la Yesu kufanya kazi kwa mtu fulani: haki. Ni kwa haki ipatikanayo kwa jina la Yesu tu ndiyo iwezayo kulifanya jina hili-hili la Yesu kufanya maajabu kwako. Kwa maana lazima tuelewe kuwa ni kwa kupitia Jina la Yesu Kristo tunapata msamaha wa dhambi

Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.” – Mdo 10:43

Wakati Petro ameamrisha mtu kilema kutembea katika Jina la Yesu. Alitembea mara moja. Kwa nguvu iliyoko ndani ya Jina hili, Yesu, ninakuamuru wewe usomaye hapa kupokea Ukombozi wako kuanzia sasa nakuendelea. Jina la Yesu Kristo lina upako, kama Biblia isemavyo:

Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda.” – Wimbo Ulio Bora 1:3

Ndiyo maana Jina hili huvunja nira za ibilisi na huleta Ukombozi kwa walio kandamizwa. Kuna kijana mdogo Mkiristo alikuwa anasafiri kwa boti siku moja, wakati boti lilitaka kupinduka akapiga kelele Yesu. Mkono usioonekana ukaja kumuokoa. Ninakuombea kuwa Jina la Yesu lianze maajabu kwako tangu leo kwa kadri unavyoliamini katika Jina la Yesu. Shetani anaweza kukukatalia chochote lakini si kwa Jina la Yesu Kristo. Kwa sababu Mungu kampa jina lipitalo majina yote.

Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.” – Wafilipi 2:9-11.

Siri nyingine ya kuweza kulifaidi hili jina ni ukiri wako kwamba Yesu Kristo ni Bwana. Ukifanya tu hivyo na kuamini kuwa alifufuka basi wewe utaokoka (Warumi 10:9)

Mathayo 1:21-23 “Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. 22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, 23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.”

CHUKUA HATUA: Tumia Jina la Yesu katika kila hali inayokuchanganya, au jambo lolote linalowakilisha mlima katika maisha yako, utaona linakupa utukufu wa Mungu Baba.

Toa Maoni yako / Leave Your Comment:

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s